Deogratias Mutungi
Senior Member
- Oct 1, 2019
- 140
- 181
Salaam Wana JF.
Kama mzalendo wa taifa hili kuna jambo nimeliona la kipekee kutokana na utawala mpya wa rais wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi, Utashi, sera na falsafa zake zinazofanyika kwa sasa bila shaka zinaweza kuivusha Zanzibar katika daraja la uchumi imara na bora kwa Afrika na dunia kwa ujumla, Ukirejea historia ya Lee Kuan Yew miaka ya 1956 wakati anaingia madarakani alikuwa na falsafa, maono na utashi wa kuifanya Singapore kuwa taifa la kipekee lenye nguvu za kiuchumi duniani, wapo waliopinga sera zake lakini badae wakakubaliana na matokeo ya sera na mifumo yake kiutawala.
Ukweli upo wazi kuwa mwanzo wa Dkt. Hussein Mwinyi katika utumishi wake kwa Watu wa Zanzibar ni wa kimapinduzi na wenye fikra za kiuchumi kama alivyokuwa Lee kwa taifa lake la Singapore, tutegemee uchumi imara wa vitu na watu ndani ya watu wa Zanzibar, Mantiki kuu ikiwa ni falsafa za utendaji aliouonyesha hadi sasa, Dhamira ya Mwinyi ni chanya katika utumishi wa watu wa Zanzibar, ni imani ya andiko hili kuwa kwa kipindi cha miaka mitano tutaiona Zanzibar yenye neema na fursa za kiuchumi na hivyo kuwa kivutio cha watu wa bara na duniani kote kuja kuwekeza Zanzibar, Naiona Zanzibar salama mikononi mwa Mwinyi, Kama ilivyokuwa Singapore salama mikononi mwa Lee Kuan Yew.