Zao la Vanilla

Zao la Vanilla

OllaChuga Oc

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2016
Posts
21,569
Reaction score
24,812
Wakuu kwema? Hili zao la vanilla nimeona linapigiwa chapuo sana hasa kwenye bei yake nasikia ipo juu sana hadi kufikia usd 500 kwa kilo. Je ni kweli?

Kwa wadau wanaohusika na ulimaji au wenye uelewa wa hili zao waje watupe elimu kuhusu ulimaji wa hili zao. Mimi siyo muumini sana wa fursa zinazotangazwa mnoo kama hii ya hili zao maana nimesikia kuna kampuni huko Njombe ndo inahusika na usimamiaji na utafutaji wa soko.

Wewe utaenda na mtaji wako wao wanakupa shamba then unaanza kulima. Je hili zao kweli ina dili?? Maana huko kagera pia na Zanzibar huko kuna wakulima pia.

Karibuni wakuu tupeane elimu kuhusu hili zao na gharama zake na ni kwa muda gani hadi unavuna na kuingiza sokoni.

Ni hayo tu wakuu..
 
Unaweza ukatoa ufafanuzi kidogo juu ya gharama hizi? Je, inawezekana kulima zo hili kwa kutumia vitalu, yaani green houses?
Mkuu kwa heka moja huwa inachukua muda gani hadi uvune? Na bei yake inakuwaje?
 
Zao la Vanilla halina gharama kwenye ulimaji kama wadau wanavosema hapo juu, gharama yake ni kwenye kuchukua muda mrefu mpaka kuvuna mwaka hadi miaka miwili kutegemeana na rando.

Vile vile kuna uzushi, sijui ni rumors za wale jamaa wa ITV wanajitangaza kuwa vanilla Kilo moja ni Shilingi milioni moja kitu ambacho sio kweli. Vanilla ina bei lakini hata soko la nje haijafika milioni moja, Madagascar ambao ndiyo soko kubwa vanilla kavu isiyo mbichi kule saivi ni dola 150$ au 180$ kwa kilo moja.

Vanilla huuzwa kwa grade na hapa bongo bei ya Vanilla iko chini sana Vanila inayouzwa hapa bongo wengi wanauza mbichi ambapo kwa bukoba vanila mbichi kilo moja ni Shilingi elfu 30.
Wanunuzi wengi wananunua mbichi.
 
Kumbe bongo bei bado ipo chini? Na hizo bei za usd 500 hazina uhalisia wowote? Na nikitaka kununua kwa huko bukoba unaweka juani tu zinakauka na solo lake la nje unauzaje? Kwa mfano kule iringa wanadai kuwa huchukua hadi miezi mitatu kuvunwa ..hiyo ni kulingana na nilivyosikia kwenye radio.
 
Ngoja leo nikujibu, kwenye jukwaa la Arsenal uwa na ku-ignore. Unaweza kupanda na ukavuna ndani ya mwaka mmoja, inategemea na urefu wa lando unalopanda, kiwango cha moisture, kivuli na mbolea. Ingawaje mwaka wa kwanza mavuno yatakuwa kidogo. Kama limelishwa na kupata matunzo mazuri eg shadding, baada ya miaka 3 mche mmoja unaweza kukupa mpaka kilo 8. kwa bei sasa unaweza pata 20,000- 30,000x8 shilingi kwa kila mche. Mimi sasa hivi nipo shambani naoanisha maua.
 
Hahahaha sawa sawa mkuu ..dah ebwana wee hongera sana mkuu shamba lako liko wapi mkuu napenda kuja kutembelea huko nione namna unavyofanya mkuu? Maana natamani sana kulima hili zao natumaini utakuwa na uelewa wa kutosha kuhusu kulima hili zao mkuu.
BTW hongera sana mkuu..
 
Kaka zile ni hadithi tu za wale jamaa wa njombe kwanza amna vanilla inayokomaa kwa muda wa miezi mitatu isipokuwa vanila huanza kuchavushwa maua kuanzia mwezi wa sita toka kupandwa na pollination yake ni mkono amna wadudu wala upepo ni wewe unahamisha mbegu kwa maua yaani ni hand pollination.

Lingine ni kuwa Vanilla huwa ikiwa mbichi ili kuwa vanila kavu kuna usindikaji hufanyika na kisha kuanikwa, vanilla hupitia usindikaji ili upate kavu na kuna vigezo vyake.
Vanila huchumwa shambani kwa vigezo pia ukikosea kuchuma au ukapitiliza muda unapata low grade. Vanila mbichi ni ile ambayo haijasindikwa na huuzwa kwa grade.

Hapa Tanzania sehemu kama bukoba wanunuzi wengi hununua vanila mbichi sababu wanasindika kwa vigezo vyao wanavovitaka.
Madagascar unaweza kuexport vanila kavu ukapata soko kirahisi.

Kwenye Swala la bei ya Vanilla kilo moja siyo Milioni moja na hata nje hiyo bei haijafika, Japo ni kweli Vanilla iliwahi kuuzwa Shilingi milioni moja na zaidi kwa kilo kwa madagascar tu mwaka 2019 nadhani ilihadimika. Kwa Tanzania vanila kavu iliuzwa shilingi laki 4 mpaka 6 kwa kilo mwaka 2019 na Uganda walinunua sana laki 4 kwa kilo kule bukoba.

Hawa jamaa wa njombe wanawachota watu akili kwamba walimiwe inaweza rudi tena kama 2019 wanaishi kwa historia na siyo reality ya sasa kilo ni 30K kwa bukoba vanila mbichi anaye bisha na abishe.
Vanilla haijawahi kuuzwa Shilingi milioni moja hapa bongo believe it or leave it.
 
Ukipata gepu lake na ukavumilia muda wake mpaka kuvuna wewe lima tu mkuu,utavuna kwa muda mrefu sana.
 
Hahahaha sawa sawa mkuu ..dah ebwana wee hongera sana mkuu shamba lako liko wapi mkuu napenda kuja kutembelea huko nione namna unavyofanya mkuu? Maana natamani sana kulima hili zao natumaini utakuwa na uelewa wa kutosha kuhusu kulima hili zao mkuu.
BTW hongera sana mkuu..
Karibu, nitaku-PM kukuelekeza nilipo
 
Ngoja leo nikujibu, kwenye jukwaa la Arsenal uwa na ku-ignore. Unaweza kupanda na ukavuna ndani ya mwaka mmoja, inategemea na urefu wa lando unalopanda, kiwango cha moisture, kivuli na mbolea. Ingawaje mwaka wa kwanza mavuno yatakuwa kidogo. Kama limelishwa na kupata matunzo mazuri eg shadding, baada ya miaka 3 mche mmoja unaweza kukupa mpaka kilo 8. kwa bei sasa unaweza pata 20,000- 30,000x8 shilingi kwa kila mche. Mimi sasa hivi nipo shambani naoanisha maua.
Sawa rando likiwa kubwa 100m utawahi kuvuna na mmea mmoja hutoa nusu kilo au kilo mwaka wa kwanza na kuongezeka hivo hivo mpaka na mpaka. Wewe upo mkoa gani?
 
Back
Top Bottom