Zari alala kwa mama Diamond

Zari alala kwa mama Diamond

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Imefichuka ,Mrembo wa Uganda ambaye kwa sasa ndiye ' usingizi ' wa Mbongo Fleva , Nasibu Abdul ' Diamond ' , Zarinah Hassan ' Zari ' hivi karibuni alitua Bongo na kulala nyumbani kwa mama wa Diamond , Sanura Kassim ' Sandra ' , Sinza- Mori jijini Dar . Mrembo wa Uganda , Zarinah Hassan ' Zari ' .

Chanzo makini kilicho karibu na familia ya Diamond kimepenyeza ' ubuyu ' kuwa , Zari alipata fursa ya kupiga ' mbonji ' nyumbani hapo alipomtembelea Diamond .

"Alikuja akambonji kwa mama Diamond kama siku mbili hivi halafu wakaondoka wote wakati Diamond alipokwenda Nigeria kwenye shoo ya Mwanasoka Bora wa Afrika 2014 .

"Awali, Diamond alitaka akamlaze Hotelini lakini mtoto wa kike akakataa , akasema anataka kuangusha usingizi nyumbani kwa mkwewe , Diamond akasema ruksa mama , " kilisema chanzo hicho .

Kikizidi kumwaga data , chanzo kilisema , mbali na kulala, Zari alishiriki Kazi za ndani ikiwemo kupika na kupakua kama ilivyokuwa kwa zilipendwa wa Diamond , Penniel Mungilwa ' Penny ' na Wema Sepetu .

Alipoulizwa Diamond kuhusiana na suala hilo hakutaka kufafanua mengi zaidi ya kukiri kwamba mrembo huyo alikuja Dar na kuondoka naye . Zarinah Hassan ' Zari ' akiwa na ' Diamond Platnumz' .

"Wewe jua alikuja , nikaondoka naye hayo mambo mengine siwezi kuyazungumzia , " alisema Diamond . Amani lilipomtafuta mama Diamond kwa njia ya simu hakupatikana lakini mtu wa karibu alisema kwa sasa hatumii simu kwa sababu ambazo hazikutajwa .
 

Attachments

  • 1421332076282.jpg
    1421332076282.jpg
    45.8 KB · Views: 1,627
Alilala kwa mama domo na kunya je, alikunya wapi? Hili jukwaa la udaku ni shiiidah!
 
Back
Top Bottom