ZARI: Hakuna kitu ninachokipenda katika maisha yangu kama kuzaa

ZARI: Hakuna kitu ninachokipenda katika maisha yangu kama kuzaa

Steven mushi mushi

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2016
Posts
533
Reaction score
739
Wakati mabinti wengine wakijikita katika matumizi ya mikorogo na kukimbilia wanaume wenye pesa hali ni tofauti kwa mwanamama zari hassan (the boss lady ) ambaye amekiri wazi kuwa kitu anachopenda zaidi katika maisha yake ni kuzaa.

Zari ambaye ni mpenzi wa mwanamziki nyota Africa diamond platnumz amesema hayo ikiwa ni siku chache tangu apate mtoto wa kiume aliyezaa na diamond ambaye watu walimbeza kuwa anazaa bila mpangilio eti kiza tu alibeba ujauzito kabla ya mtoto wao wa kwanza tiffah hajatimiza mwaka mmoja.

Licha ya zari kuwa na watoto watano kwa sasa ameweka wazi kuwa kwa sasa yeye na diamond wana mpango wa kuzaa mtoto mwingine wa tatu na baada ya hapo hatozaa tena na badala yake watajikita zaidi katika kuwalea watoto wao.
 
Diamond alishasema anataka watoto wasiopungua 5 au 6... Mwakani December nadhani tutapokea mdogowake nillan..
 
  • Thanks
Reactions: MC7
McKan: Ohh no, Tom is not reachable. He should know about this. Anyway, this is what you are good at.
 
Labor wards ambassador,kuzaa sana nacho kipaji.
Mimi nimezidisha sana watatu tu.
Hongera zake.
Pole sana...
Kuna zile wanaita bahati mbaya hakutarajia..... huku wa kwanza anamiezi 6'unusu. Then Kitu na Box ya watoto pacha wanne!!.
 
Usije kushangaa watatu wakawa sita, maana kila ukiwaangalia unasema 2 pairs is okay huyu mwingine yuko peke yake peke yake sana, ngoja niongeze mmoja mwingine ukijastuka una watatu wengine. Chezeya utamu weye!

Labor wards ambassador,kuzaa sana nacho kipaji.
Mimi nimezidisha sana watatu tu.
Hongera zake.
 
Huyo anapenda sana KUCHAPWA NAO.. sio kuzaa... Mwanamke gani huyu...
 
Nadhani la muhimu ni kuhalalisha mahusiano tu, maana Khadijah mke wa Mtume Muhammad alikuwa na watoto 11 kwahiyo naona Zari watoto 5 ni wachache sana, as long as anajiweza kiafya na kipesa watoto waje tu..!!
 
Huyo nae anatumia watoto kama mtaji , chezea child support , eti anapenda kuzaa why hakuzaa na yule mwanamme wake choka mbaya mwenye sixpark?baada ya kutengana na mme wake , kabla hajampata diamond why hakuzaa na hao wanaume?
 
Back
Top Bottom