Zawadi Bora Niliowahi Kupokea

Mtayarishaji

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2012
Posts
291
Reaction score
198
Binti mwenye umri wa miaka 13 alihisi hivyo baada ya kupokea zawadi ya mnyama anayempenda.

Mwanamke fulani ambaye ni mfanyabiashara mwenye mafanikio alisema kwamba zawadi ya kompyuta aliyopewa na baba yake alipokuwa shule ya sekondari, ilibadili maisha yake.

Mwanamume aliyeoa hivi karibuni anahisi kwamba kadi aliyotengenezewa na mke wake walipotimiza mwaka mmoja wa ndoa, ilikuwa zawadi bora aliyowahi kupokea.

Kila mwaka, watu hutumia muda na jitihada nyingi wakitafuta zawadi “bora” ya kumpatia rafiki au mtu wa ukoo katika matukio ya pekee. Na wengi wao wangependa kusikia maneno kama yale yaliyo kwenye kichwa cha makala hii.

Swali

Je, ungependa kupokea au kutoa zawadi ambayo itathaminiwa?

Tarajio hilo linapendeza sana, kwa sababu ya jinsi linavyofanya mtoaji na mpokeaji wahisi. Haishangazi kwamba Biblia inasema:

“Kuna furaha zaidi katika kutoa kuliko ilivyo katika kupokea.” (Matendo 20:35) Bila shaka, tutapata furaha zaidi ikiwa zawadi tunayotoa inathaminiwa na yule tunayempatia.


Maswali ya Kutafakarisha

Hivyo basi, unapotoa zawadi, unaweza kufanya nini ili wewe na yule anayeipokea mpate furaha zaidi?

Na ingawa si rahisi kutoa zawadi “bora,” unaweza kufanya nini ili zawadi yako ithaminiwe?
 
Kuna mdada nilimpa zawadi ya kitombo heavy mpaka leo uwa anaikumbuka iyo zawadi
 
Zawadi bora niliyowahi kupokea ni kuzaliwa, kutunzwa na kupewa msingi mzuri hadi kuwa na maisha bora leo. Natamani niwashukuru wazazi kwa namna fulani kila siku.
 
zawadi bora kabisa OXYGEN ya bure maana ingekuwa inauzwa na nilivyo bahiri nahisi ningekubali nife tu kuliko kununua kila siku
 
Kuzaliwa nikakua na kujitambua ni Zawadi tosha kwangu.
Mengineyo Yesu Kristo atanibadilisha tu, maana ndiye niliyemchagua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…