Zawadi gani nzuri kwa mwenzi wako

Zawadi gani nzuri kwa mwenzi wako

sulphadoxine

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Posts
2,257
Reaction score
649
Je! ni zawadi gani nzuri ya kumpa mwenzi wako?????????
Hili swali naona kama tunategana, maana ukweli watu siku hizi wanapenda fedha zaidi. Sawa unaweza kumpelekea ua, unaweza kununua nguo na vitu vingine, lakini watu wanapenda fedha.

Zawadi ifaayo katika maisha ya ndoa ni kupendana kwa dhati na kufanyiana mambo mazuri. Mheshimu mwenzi wako, na endelea kubuni mambo mazuri ya kumfanyia. Kama kweli unampenda, ni wazi hutapenda awe mnyonge.
Katika mapenzi kila mwanandoa anapaswa kufahamu kuwa analo deni la kumpenda na kumfanyia mema mwanandoa mwenzake.

Unaweza ongozea majibu.................
 
Mi nafikiri upendo wa kweli huleta heshima na amani ndani ya nyumba na kujenga mapenzi mazito. Zawadi hugeuka kuwa kama kachumbari kwneye mapenzi ktk harakati za kunogesha uhusiano wenu
Wadada wengi hupendelea zawadi kama mikufu, saa, nguo za ndani, cheni, hereni nk contrary na sisi wanaume ambao zawadi yeyote kwetu poa.
Ni vzr kusoma na kujuana interest zenu ili zawadi mpeanazo ziwe na maana zaidi ...
Ni hayo tu wana JF!
 
geen wanitoa udenda........
@DR jamani huo udenda umepita wapi wakati mdomo wako umeweka plaster za kutosha hivyo, usikute na mikono imefungwa kabisa sasa geen akitokea kaka huna la kufanya, itabidi bujibuji apite hapo kwa bahati mbaya aone unvyombwela kwa kufurukuta, hapo ndo geen atapoana kilio na kusaga meno.
 
Kumbe ulikuwa unauliza swali na majibu unayo!
!@#$%^&@#$%^&

Je! ni zawadi gani nzuri ya kumpa mwenzi wako?????????
Hili swali naona kama tunategana, maana ukweli watu siku hizi wanapenda fedha zaidi. Sawa unaweza kumpelekea ua, unaweza kununua nguo na vitu vingine, lakini watu wanapenda fedha.

Zawadi ifaayo katika maisha ya ndoa ni kupendana kwa dhati na kufanyiana mambo mazuri. Mheshimu mwenzi wako, na endelea kubuni mambo mazuri ya kumfanyia. Kama kweli unampenda, ni wazi hutapenda awe mnyonge.
Katika mapenzi kila mwanandoa anapaswa kufahamu kuwa analo deni la kumpenda na kumfanyia mema mwanandoa mwenzake.

Unaweza ongozea majibu.................
 
Zawadi nzuri ni ile atakayo itaka na niweze kumpa,...
Ila isiwe roho yangu au ya mtu yeyote.
 
Back
Top Bottom