Salamu sana wana cc wote;
Salamu sana wageni wote mtakaosoma huu uzi.
Leo nimekuwa natafakari sana kuhusu zawadi;
Nikajikuta najiuliza .......... hivi ni zawadi gani ya thamani kubwa ambayo
nimewahi kumpa mtu ..............
Kipekee nimekumbuka kuwa niliwahi kuwapa rafiki wawili wa karibu zawadi;
Ni zawadi ya thamani kubwa, sijui kama wao waliichukuliaje.
Hata mimi nimewahi pia kupewa zawadi kadhaa wa kadhaa, nyingi nazikumbuka mpaka leo;
Je, wewe mwana jf umewahi kumpa au kupewa zawadi na rafiki, ndugu, mzazi au mtu unayemfahamu.
Na hiyo zawadi umeichukuliaje?
Naamini kuwa lugha hii itaeleweka, nichukulie tu kama nisiyekijua kiswahili vizuri.