Pre GE2025 Zawadi ya kimkakati: Mbunge wa Viti Maalum Stella Ikupa agawa kompyuta 34 kwa Jumuiya Ya Wanawake wa CCM

Pre GE2025 Zawadi ya kimkakati: Mbunge wa Viti Maalum Stella Ikupa agawa kompyuta 34 kwa Jumuiya Ya Wanawake wa CCM

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wanabodi,

Hivi kweli kwenye nchi ambayo wanafunzi wanakaa chini na hawana hata vyoo huko mashuleni, mtu ambaye umeaminiwa na wananchi na wanawake wenzio kweli unaenda kugawa computers huko CCM?

Wakati napita napita huko mitandaoni nimekutana na clip ya Mbunge wa Viti Maalum Stella Ikupa, akiwa anagawa jumla ya tarakilishi (computer) 34 kwa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT).

Soma pia: Mbunge Samizi amuunga mkono Rais Samia kwa kugawa majiko ya gesi 400. Wananchi wamchukulia fomu

Tarakilishi hizo zimekabidhiwa rasmi kwa Katibu Mkuu wa UWT, Ndg. Suzan Peter Kunambi (MNEC), ambaye atazisambaza katika ofisi za Makao Makuu ya UWT pamoja na mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar.

Kwanini hizi computers kama kweli ana moyo huruma asingezipleka mashuleni au hata kwenye zahanati za vijiji? Au ndo takrima anatoa kwa CCM wenzie ili kuelekea mwaka 2025 apite kiurahisi kwenye kura za maoni?

CCM mna shida gani?

 
Back
Top Bottom