Hivi kweli kwenye nchi ambayo wanafunzi wanakaa chini na hawana hata vyoo huko mashuleni, mtu ambaye umeaminiwa na wananchi na wanawake wenzio kweli unaenda kugawa computers huko CCM?
Wakati napita napita huko mitandaoni nimekutana na clip ya Mbunge wa Viti Maalum Stella Ikupa, akiwa anagawa jumla ya tarakilishi (computer) 34 kwa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT).
Tarakilishi hizo zimekabidhiwa rasmi kwa Katibu Mkuu wa UWT, Ndg. Suzan Peter Kunambi (MNEC), ambaye atazisambaza katika ofisi za Makao Makuu ya UWT pamoja na mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar.
Kwanini hizi computers kama kweli ana moyo huruma asingezipleka mashuleni au hata kwenye zahanati za vijiji? Au ndo takrima anatoa kwa CCM wenzie ili kuelekea mwaka 2025 apite kiurahisi kwenye kura za maoni?