Zawadi ya kumpatia mke siku yake ya kuzaliwa

Zawadi ya kumpatia mke siku yake ya kuzaliwa

OME123

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2010
Posts
1,497
Reaction score
605
Naombeni mnisaidie hivi ni zawadi ipi nikimpatia mke wangu itakuwa poa. Nataka nimpeleke suprise ya zawadi.

Je, nikimpatia kama 100,000 inaweza kuwa sawa au nimnunulie kitu .na je iwe kitu gani?
 
Zawadi kama nini bro.nisaidie wazo
 
Mnunulie kati ya handbag, shoes, saa, cheni, bracelets au nguo au nunua vyote kama msuli unaruhusu
 
Mkuu mpe pesa na maua
Mwambie pesa anunue anachovutiwa kwa muda mrefu kununua au nenda nae mahala umlipie. Ni mkeo utakuwa unajua ni kitu gani ameshazungumzia atapenda kuwa nacho yeye pekee kisicho cha kushea or kutumika na wengine hata wewe
 
Mnunulie saa.. ila isiwe saa tu tafuta saa nzuri na imara..
Kisha usiishie hapo ktk zawadi hiyo muandikie na ujumbe wa maneno mazuri na mazito.. ikiwa kama siku yake ya kuzaliwa msifu kwenye ujumbe huo pia muandikie maana ya wewe kumpatia zawadi hiyo ya saa,simamia mantiki ya kujali muda wake kuwa nawe yeye kuzaliwa kwa ajili yako pia mkumbushe kuwa muda mlionao ndio huo unaohesabika kwenye saa na ni mchache kwa maana ya tunaishi kidogo na tunakifa muda mrefu!..
Pia hiyo saa ipatie jina zuri la utani ambalo unahisi atalipenda!..
Then mtoe mahali peke yenu mkale mnywe na mstareheke vilivyo bila kusahau mkate wetu ule wa kila siku utoke ktk namna ya haja..😜
 
Back
Top Bottom