zawadi za familia kwa maharusi

MKATA KIU

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2010
Posts
3,410
Reaction score
8,184
Heshima kwenu brothers and sisters

nilikuwa nachek thread ya smile ya mwanamke kwenda kwa mume na kila kitu haipendezi. Nikakumbuka na kisanga nilichokutana nacho kwenye harusi ya xul mates,

Wazaz wa upande wa kiume ( mama ) alitangaza kama mzaz anawazawadia maharusi milion 30 za kuanzia maisha na gari ndogo yeyote watayotaka isiyozidi million 15 akadai hiyo ni zawadi yake mama kama mama baba wa bwana harusi atatoa ya kwake peke yake akirudi maana alikuwa na uzuru nje ya nchi,

Baada ya mama kumaliza baba wa bibi harus naye akasimama na kusema familia yake inawazawadia ngombe mmoja wa maziwa, aliisema hiyo zawadi kinyonge sana as mama wa bwana aliongea kwa mbwembwe nyingi

Wadau tusaidiane haya mambo ya kutangaza zawad hadharan harusin ni sawa?
 
kimsingi ni misifa tu...mimi kwenye harusi yangu hakuna ishu za kiswahili kama hizo kupewa kipaumbele
 
kiistarabu si sawa....kihaya ni sawa

Cha kushangaza sio muhaya huyo mama, ni mtu wa iringa,, yaan haikuwa na uhaya hata kidogo na inasemekana hiyo harusi watairusha tbc soon walifanya cleopatra quality centre mwez wa 6 mwishon
 
Huu ustaarabu wa kutangaza zawadi kwa kadamnasi sijui umetokea wapi.

Wewe mama au baba kwa kunadi huko zawadi unapata faida gani?

Haipendezi, sana sana ni ria tu
 
kila mtu anajikuna anapoweza, haina haja kuwa mnyonge coz kila mtu na kipato chake
 
kuna ndoa ilivunjika sababu ya zawadi. kamati imetangaza wanampa bwana harusi gari kumbe hawana hela ya zawadi, wameongea na mshkaji kuwa tutazuga tu.
waliporudi home bibi harusi anadai gari walilopewa zawadi, akapigwa kiswahili kuwa zile zilikuwa mbwembwe tu, kwani alielewa................... akasema lazima gari umehonga kwa uliyetaka kumuoa ukampiga chini, sasa ndoa inaeshia hapa, nenda kwa uliyempa gari.
Kuna zawadi kweli zinakuwaga, lakini sidhani kama ni ustarabu kuzitamka kwa MISIFA. ila kuna zawadi najua nyingi tu huwa hazipo, zinatamkwa tu
 

Hizo kweli zipo but kwa familia ya jamaa hela zipo, tena za kutosha tu,

Waliosoma feza boys class of 2003 wanamjua kama "wa kishua" kwa mtu aliyepita hiyo shule na imani ameshajua tunamuongelea nani
 
Hizo kweli zipo but kwa familia ya jamaa hela zipo, tena za kutosha tu,

Waliosoma feza boys class of 2003 wanamjua kama "wa kishua" kwa mtu aliyepita hiyo shule na imani ameshajua tunamuongelea nani
kila la heri kwa hiyo ndoa "ya kishua"
 
hao wanatakiwa waoane wa style hiyo wote ili mashindano yanoge otherwise huwawanatutesa wenzao.
 

Kwa mtazamo wangu, suala la kutangaza zawadi nimelisikia kwa kipindi kirefu sana. Na kwenye harusi nyingi nilizohudhuria mimi, nimeona wakitangaza zawadi kwa mbwembwe nyingi hususan zawadi hiyo inapoonekana ni kubwa. Binafsi, sijui utaratibu huu ulianza lini na ni nani aliaanzisha mpaka ukafikia hatua ya kuchukua kasi na kuzoeleka ktk baadhi ya mahurusi kana kwamba ni fashion au ni mojawapo ya taratibu za kukamilisha sherehe za harusi.

Nimefikiria na napenda kutoa maoni kuwa utaratibu huu kwangu nauona kama hauko sawa kwa maana unaweza kuleta utofauti wa hali za kiuchumi za familia mbili zinazounguana mbele ya jamii iliyoalikwa kwenye harusi na hivyo kujenga hali yakudharauliana kati ya hizo koo mbili na hivyo kupunguza mahusiano mazuri na kuzifanya ndoa na mahusiano ya hizo koo mbili ziwe ktk hali ya mashaka baada ya tukio.

Nafikiri wakati umefika wa kubadilika na kuachana na taratibu ambazo kimsingi hazina faida ktk karne hii tuliyonayo. Nakushukuru mtoa mada kwa kulileta hili jamvini.
Asante.
 
well cdhani km kulikua na haja ya kutangaza hzo zawadi coz twaz jus the matter of telling the two PRIVATELY kwmba watapewa zawad flan, but hapo upande wa Bi harusi lazima waji feel Inferior compare na zawadi walotoa wao. There is no need kwakwel
 
ni misifa ya siku hizi ......tena ukutu upande wa pili hakuna kitu inasononesha jopokuwa ndio maisha
 
HorsePower harusi za siku hizi kila kitu usani kuanzia ndoa zenyewe hadi zawadi.....ukiangalia siku za nyuma ulikuwa unaweza kuandaa harusi kwa gharama ndogo siku hizi mbwembwe kibao gharama inafika ya kujenda nyumba ni mashindano kila kukicha
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…