Ni kweli kuwa TBC hawajajipanga na comedy kwa kuwa suala la akina Masanja kwenda TBC lilikuwa kishabiki zaidi. Hata hivyo TBC wana mawazo mengi ya kibiashara na kimaboresho. Ukiangalia kutoka TVT hadi TBC kumekuwa na mabadiliko makubwa sana. Angalia vipindi vyao na Graphics zimeboreshwa. Ila suala la comedy mbadala unakuwa mgumu sana. EATV pia watakuwa na shida kupata mbadala. Hata akina Bambo si mbadala muafaka. Walichoangalia actually si kufanya comedy ila ni kuwa na tukio litakaloaminika kutazamwa na wengi na kisha kuvuta matangazo (biashara).
Clouds ni namba nyingine Mkuu. Nakerwa na tabia yao ya ki-CCM CCM. Naichukia CCM. Ila Clouds wana uwezo mkubwa kuibua vipaji. Angalia watu waliopitia Clouds Jide, Fina, Masoud, Amina, etc. Angalia ambao bado wapo. Angalia matamasha. Angalia clouds TV, vipindi na graphics. Angalia talents na bidii za viongozi Ruge na Kusaga. Angalia investments na initiatives zao zingine. Nauchukia u-CCM wao, napenda bidii zao.