kama kweli TBC wanafikiri wana haki na Ze Comedy si waanze kuwatumia kama Ze Comedy halafu waone kama hawatafilisiwa hadi senti ya mwisho?
Mzee Mwanakijiji,
Hilo wanalifahamu ndio maana hawajaanza!!!
Huyo ndiye MENGI tunayemfahamu baadhi yetu inapokuwa ni kuchagua kati ya PESA na WATANZANIA. Yeye aliwalipa nini RTD alipowachukua kina BROTHER MIKI, NYAISANGA, CHARLES HILLARY, MAJURA, ... Wakaenda wakaanzisha vipindi vinavyofanana na vya RTD na vikarushwa katika MUDA uleule. Lakini, WASANII wetu jifunzeni sana katika hili.
basi inabidi rtd wangedai hakimiliki ya muda...?Karibu kila muda wa TAARIFA YA HABARI ya RTD, RO nao waliweka muda huohuo; kipindi cha MICHEZO RTD, RO wakaweka muda uleule wakakiita SPOTI LEO; kipindi cha ZILIPENDWA RTD Jumapili, RO nao wakaanzisha muda huohuo,...
.....Jamani mnajua huenda hata hawa watoto wa ze comedy hilo bifu la Mengi na Manji walikuwa hawana ahabari nalo lakini ndio jumba bovu limewaangukia wao.. Mi nadhani wazo la kwenda mahakamani sio zuri sana ukizingatia kuwa hapa ni vita ya matajiri wao ndio wanaoathirika na huenda walikubali kufadhiliwa na Manji wakiamini atawabeba kulingana na ndoto zao.Kasheshe upande mwingine, ni hawa watu wa TBC na EATV wangekaa pamoja na kuona how they could reach a compromise bila kuwaharibia hawa vijana. Binafsi naamini tatizo la Ze Comedy limeingia baada ya Manji kuingilia kati. Kama ingekuwa kati ya TBC na EATV ingekuwa ni rahisi sana kwa haja jamaa kukaa pamoja.
Hawa wa Ze Comedy kukubali kutumiwa na Manji wakati wametoka kwa Mengi nadhani ilikuwa ni lack of judgement au ushauri mzuri. Maana hata kama Mengi angetaka kuwaacha waende TBC, ni wazi hayuko tayari kumuacha Manji avune asichopanda.
Karibu kila muda wa TAARIFA YA HABARI ya RTD, RO nao waliweka muda huohuo; kipindi cha MICHEZO RTD, RO wakaweka muda uleule wakakiita SPOTI LEO; kipindi cha ZILIPENDWA RTD Jumapili, RO nao wakaanzisha muda huohuo,...
NO NO NO.
wanunue wakati ni majina yao halisi toka zamani tunamjua Joti,Mpoki sasa wanunue vp?Na jina si hilo wamebadili wanaitwa ZEE COMED.