ZE COMEDY ya EA TV

Tiger

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2007
Posts
1,747
Reaction score
386
Kwa wanaofuatilia,
naomba kufahamu, wale jamaa(ze comedy ea tv) wanaendelea na kipindi au imekuwaje?
Nakumbuka kile kipindi wakiwa wanatafuta washiriki mambo yalikuwa hot kwelikweli
maana waliamua kuweka ratiba moja na akina Masanja.
Nimejaribu kufuatilia lakini siwaoni hewani akina Bambo.
Kama kuna anayefahamu, naomba anifahamishe.
 
Jiandae kufuatilia vipindi vya ZE KOMEDI kupitia EA TV kuanzia alhamisi ya tarehe 23 Septemba.
Sijui watakuja na kitu kipya au ni yaleyale ya ORIJINO KOMEDI.
tusubiri tutapata majibu
 
Kwa waliofuatilia jana watujuze... Maana ALUUUUU!! Imepitwa na wakati... Sasa hvi kuna msemo mpya... "Heshima yako inashukaaa"
 
Hivi Ze Comedi wa TBC wanamaanisha nini wanaposema "heshima yako inashuka"
 
Sidhani kama wataweza kuwafikia wale wa tbc japo hawa watbc nao hawajafikia viwango walivyokuwa navyo eatv
 
Sidhani kama wataweza kuwafikia wale wa tbc japo hawa watbc nao hawajafikia viwango walivyokuwa navyo eatv
Tusubiri watakapoanza ndipo tutawajaji vizuri!
 
vita ya mengi ndio imeharibu ladha ya comedy, ila bado pae TBC na jamaa wa STAR TV wanafanya vema
 
Kingwendu baridiiiii na bambo moja lililojaa
 
Wamefulia! Wakakae nyumbani!

Huo ni mtazamo wako na pengine wewe si mlengwa, jamaa wanajitahidi kwa kiasi kikubwa ila tu siku moja moja wanakuwa hawana vitu vya kuvutia sana kama ambavyo sehemu nyingine dunia zenye comedy hutokea siku kipindi kisivutie sana, inapotokea huwezi sema wamefulia, lets be positive penye ukweli
 
:mad2:comedy bongo!!!!!!! mh!
Bado sijaona,hawa wote wa TBC na EATv wajaribu kuona nchi zilizoendelea wanafanyaje, kumchekesha m2 si lazima kuvaa sketi au kulia kama mtoto
:confused2::confused2:
 
Hii tabia ya kuwadiscourage wasanii, mnainunua wapi, na kwa gharama gani?. Waliondelea hupongeza kwanza and then kutoa maoni kwa busara, sio kuponda MWANZO MWISHO. We've 2 change.
 
me niliiangalia kidogo wala sirudii tena hawana ubunifu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…