Kamanda Moshi
JF-Expert Member
- Apr 1, 2012
- 1,928
- 2,867
Wakuu, natumaini mu wazima na kwa wale wenye changamoto za afya na mengineyo nawapa pole na kuwatakia uponyaji wa haraka!
Wakuu kuna hii changamoto ya Askari police 👮‍♀️ kugeuza kivuko cha waenda kwa miguu sehemu yao ya kupigia hela.
Nina imani jambo hili lipo kwenye mikoa mingi na Hata humu jukwaani limekwisha tolewa taarifa na malalamiko mara kwa mara.
Nitatoa mifano miwili ambayo watumiaji wa hizo barabara watakubaliana nami kuwa sasa ni wakati jeshi la police kuchukua hatua kwa Askari wake ambao wamegeuza zebra crossing atm ya kuchumia pesa za watanzania na kuleta kero na foleni zisizo za lazima!
1. Kivuko cha River side - Ubungo
Askari hupenda kusimama njia panda ya Ubungo maziwa ili “kuzipiga” kwa wale wanaolekea buguruni na just before fly over ya mfugale “kuzipiga” kwa hawa wanaokuja Mlimani city au Mbezi!
Eneo hili waenda kwa miguu ni wengi na wamekuwa wakivuka randomly kitu kinachofanya magari kusimama Hata kwa 10 min kusubiria mtu mmoja mmoja kuvuka! Askari huwa wapo kwa mbele wanaangalia na kusubiri ukosee kidogo wale hela!
Sehemu hii utawakuta Traffic police na pia private police wote macho yamewatoka kukusanya mapato ya mifuko yao!
Matokeo ya jambo hili, magari hayatembei na kunakuwa na foleni mpaka external au juu ya fly over, na kupoteza nia nzuri ya serikali kujenga fly over yetu kwa gharama kubwa ili kupunguza foleni.
2. Kituo cha Shule -Bagamoyo road Mbezi beach
Sehemu hii napo mambo ni Yale yalee, Askari wamekaa mbele ya zebra crossing opposite na kituo cha mafuta cha Puma wametega mingo yao! Hapa napo huwa panatokea foleni mpaka njia panda ya Goba.
Wakuu, ina maana uongozi na viongozi wa jeshi la police pamoja na wakuu serikalini hawalioni hili tatizo? Kwa nini hawa police wanaokaa maeneo hayo wasiongoze watu na magari kutumia barabara ili kuondoa foleni zisizo za lazima na kurudisha nyuma uchumi wa nchi?
Mkuu Maxence Melo nadhani haitoshi tu kwa sisi kuandika humu, tunaomba kwa kutumia influence yako hii kero ifikishwe sehemu husika na hii kero itatuliwe maana sio tu inachochea rushwa ila pia inarudisha uchumi wa nchi nyuma kwa kuleta foleni zisizo za lazima.