Zebra Crossing: Mgodi wa Trafiki na Polisi wa kawaida

Kuna hili la stand kufatana na zebra,mfano magomeni mwembechai na manzese!!umesimama kumruhusu apite anakupa ishara wewe endelea kumbe yeye ni abiria na anasubiri daladala na unafika mbele polisi wanakukamata!!hii imekaaje?
Zebra za manzese na magomeni ukipitia simama washa haZard, sikilizia kdg ndy uvuke
Wakikukakata hapo basi wana jambo
Lao si bure

Ova
 
Mradi wa AIJIPII
 
Uko sahihi kabisa kongole!!mfano tunduma kuna wakati taa zinawaka kuruhusu waenda kwa miguu na kuna wakati zinawaka kuruhusu magari!!shida ya askari hawataki kutoa elimu kwa waenda kwa miguu wao kazi ni kusumbua wenye magari tu
Mimi nilishakata tamaa na hao Jamaa kama hawajui PGO inasema nini, hebu fikiria wataweza kutoa Elimu kwa Wananchi? Zaidi ya kusuburi Ajali itokee ili waje kufungua Mgodi kwenye Wallet yako.

Mimi nimeshakata tamaa,,,nimekuwa Popo leo Bundi kesho.

Kutembea usiku Nchii hii ni Amani kuliko mchana taa za Fuso za usiku nimeshazizowea.
 
Pale majumba 6 trafiki wa pale walikuwa wanaiyo tabia sana ..kama unatokea Kinyerezi ukifika tu pale mataa ya majumba 6 kulikuwa na zebra imefifia kabisaa basi ukisogeza tu tairi ..jamaa haooo
 
Umeyasema yote ndugu, umetoa mifano dhahiri, ila pia Kuna zebra crossing nyingi zenye hili tatizo, Kwa mifano Mlimani City, Kona ya Mwenge kuelekea Tegeta na kwingineko kwingi, huwa najiuliza inakuwaje wakati mwingine hadi askari mwenye nyota anakuja kulinda taa au Zebra crossing!?? Hivi askari ni wengi hadi wanafanya kazi hii!? Unaweza kukuta kutoka Mwenge hadi Tegeta unakutana na Police check point 5, yenye askari 6 kila point, najiuliza je Kuna hitajio lote hili!? ( Hao jumla Yao ni 30) Hili tatizo ni kubwa sana Kwa wanaotumia barabara kujipatia riziki, naamanisha wanaoendesha Magari ya kibiashara Fikiria Carry inatoka Mwenge hadi Tegeta check point 5 atawapa nini wote Hawa!? Daladala usiseme, tipper trucks na kadhalika!! Sijajua Kwa nini jeshi letu pendwa la polisi limeamua kufanya hivyo!? Wabunge wetu wapendwa walipoona Kadhia imekuwa kubwa wao walitaka wapewe namba plates za kujitenga!! Jamani Waziri WA Mambo ya ndani Fanya Jambo watumiaji WA barabara wamechoka
 
Kuna hili la stand kufatana na zebra,mfano magomeni mwembechai na manzese!!umesimama kumruhusu apite anakupa ishara wewe endelea kumbe yeye ni abiria na anasubiri daladala na unafika mbele polisi wanakukamata!!hii imekaaje?
Kwa kweli mkuu hii kero ya zebra ni kubwa sana. Huwa sielewi kabisa kwa nini uongozi wa police unaifumbia macho, sitaki kuamini kuwa eti hawaijui!
 
Pale majumba 6 trafiki wa pale walikuwa wanaiyo tabia sana ..kama unatokea Kinyerezi ukifika tu pale mataa ya majumba 6 kulikuwa na zebra imefifia kabisaa basi ukisogeza tu tairi ..jamaa haooo
Wanawahi kupiga mpunga
 
Mkuu nashukuru sana kwa mchango wako! Na ni kweli nyakati nyingine Hata vehicle inspector anajiunga kwenye hichi kifurushi cha zebra!
Kurundikana kwao kunatuonyesha ni jinsi gani wanavokusanya mapato ya chapchap na kwamba kwenye zebra ni deal sana!
 
Traffic anapangiwa kituo
Atatumwa hesabu apeleke
Kwa mkubwa...hyo pia ipo

Ova
 
Mkuu umesahau na zebra za city Centre karibu na peacock hotel
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…