Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Jonas Savimbi aliongoza vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Angola kwa miaka mingi na kutoa fursa kwa maliasili za nchi hiyo kumilikiwa na makampuni ya mabepari.Uraisi alioutarajia hakuupata na baada ya kumaliza kazi naye akauliwa.
Kwa upande wa Zelensky wa Ukraine wakati nchi ilikuwa na neema kubwa hakuona shida kuchukua jukumu la kuichokoza Urusi akiwa na tamaa kuitwa shujaa.
Matokeo ya kazi ya Zelensky yamekuwa ni hasi baada ya kukwaana na kisiki cha mpingo huko Urusi.Sasa baada ya kuitia umaskini na ukata mkubwa Marekani amekuwa hana thamani tena.
Raisi Trump wa Marekani ambaye kila kitu duniani anakiangalia kwa jicho la kibepari amemtangaza Zelensky kama dikteta kwa watu wake.Katika hali hiyo hakuna dalili yoyote ya Ukraine kufanikiwa katika lolote lile waliloaminishwa wangelipata.
Zaidi ya yote kiongozi wa Ukraine sasa atakuwa anaishi kwa hofu na udhalili mkubwa kwani wakati wowote Marekani inaweza kuongoza harakati za kumgoa madarakani na kumuweka mwengine ambaye angalau hatazuia madini yanayotakiwa na Trump kupelekwa huko kufidia gharama kubwa zilizotokana na vita hivyo vilivyodumu kwa takriban miaka mitatu sasa.