Zelensky: Putin hataki kumaliza vita Kidiplomasia

Zelensky: Putin hataki kumaliza vita Kidiplomasia

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema Kiev ingependa kukomboa maeneo yaliyochukuliwa na Urusi kwa njia ya kidiplomasia, lakini Vladimir Putin amedhamiria kuendeleza mapambano ya kijeshi.

Zelensky amesema baada ya uvamizi wa Urusi kuanza, Ukraine ilifanikiwa kukomboa tena zaidi ya 50% ya eneo ambalo Putin alikalia, lakini hakutaka umwagaji damu uendelee.

Soma Pia: Hatimaye Zelensky akiri hadharani jeshi lake haliwezi kuyarejesha maeneo yake yaliyokombolewa na urusi


"Hatutaki kupoteza maisha ya watu zaidi, lakini hatuwezi kukubali unyakuzi wa ardhi yetu," Zelensky amesema.

"Hatutambui uvamizi huo kisheria, lakini tunataka kurejesha eneo lililonyakuliwa kidiplomasia badala ya hatua za kijeshi, akini Putin hataki kumaliza vita hivi."

Screenshot 2025-01-29 220210.png
 
Hehe kajamaa kanatia huruma leo kanataka diplomasia.....miaka yote hio anasema hataki diplomasia atayarudisha maeneo yake kwa mtutu leo yamekua haya.. ....kwakweli hali ni mbaya ,ulikua unatapa mjini sababu una mganga mkali ghafla asubuhi unaamka unapata taarifa mganga wako kafariki.........
 
Wafadhili wa Zelensky wamekata tamaa na hii vita, mmoja mmoja anasitisha misaada kwenda Ukraine. Wale waliomshinikiza Zelensky kukataa makubaliano ya amani leo wanajitoa kumsaidia, ndio maana leo anatoa kauli hizo. Hakumbuki kuwa alipitisha tamko la kukataa mazungumzo yoyote ya amani. Huyo mchekeshaji amejikatia tamaa baada ya Trump kuingia madarakani.
 
Mbona Siku hizi sijasikia silaha mpya kuingia Ukraine toka Uingereza na Ujerumani.
 
"Huezi kuona hayo yakitokea nchi za Magharibi"

😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂

Roho mbaya, rushwa, unafiki, udikteta, ubadhirifu, vita na mauaji ya halaiki. Dunia ni kijiji kilicho kiganjani.


##########

Wazungu bana.
 
Wafadhili wa Zelensky wamekata tamaa na hii vita, mmoja mmoja anasitisha misaada kwenda Ukraine. Wale waliomshinikiza Zelensky kukataa makubaliano ya amani leo wanajitoa kumsaidia, ndio maana leo anatoa kauli hizo. Hakumbuki kuwa alipitisha tamko la kukataa mazungumzo yoyote ya amani. Huyo mchekeshaji amejikatia tamaa baada ya Trump kuingia madarakani.
Ndiyo maana hata kwenye mazungumzo hayupo
 
Ile propaganda kwenye radio na tv Ukraine is winning vimeishia wapi?

Mataifa 51 yalitoa support kwake na kusema majeshi ya Urusi yameisha wanakodisha mamluki. Vyote vimeisha.

0ver 29% ya eneo la Ukraine limechukuliwa na over 60% ya fertile land, na eneo lenye madini na viwanda vikubwa vyote vimechukuliwa. It is estimated eneo lililo chukuliwa Lina utajiri wa over 14 Trillion Dollars.

Hivyo Putin mshindi
 
Vita huleta heshima, wapigane tu mpaka kieleweke. Wasikubali kirahisi tutakosa habrai za maana duniani.
 
Back
Top Bottom