Sikirimimimasikini
JF-Expert Member
- Dec 27, 2019
- 2,926
- 15,634
Kama ulikuwepo kipindi cha vita ya pili ya Marekani nchini Iraq (2003 - 2011), inawezekana utamkumbuka Baghdad bob, Mohammed Saeed al-Sahaf, ambae alikuwa ni Waziri wa Habari wa Iraq na wakati huo huo ni mugizaji (part-time comedian).
Hadi hatua za mwisho mbaya wa kuanguka kwa serikali ya Iraq, al-Sahaf, alikuwa akitabiri kuwa uvamizi wa majeshi ya Marekani nchini Iraq utafeli. Yaani majeshi ya Saddam (Iraq) yatashinda vita ile. Kitu kilichokuwa kikiwaaminisha wengi juu ya yale aliyokuwa akiyasema au kutabiri ktk video zake alizoposti ni ile hali ya kujiamini na ukauzu. Alikuwa anauwezo wa kubadili, ktk mazungumzo na propaganda zake, uhalisia wa kushindwa kwa majeshi ya Iraqi akaita na kuaminisha umma kuwa ni Ushindi wa majeshi ya Iraq dhidi ya majeshi ya uvamizi.
Rais wa Ukraine Zelensky, ambaye aliwahi kuwa mwigizaji kabla ya kuukwaa urais, pia nae sasa hivi anapambana na majeshi ya uvamizi ya Russia. Amekuwa akipost tweets za kishujaa na video fupi fupi tokea ktk mji mkuu, Kyiv, ambao kwa sasa unaendelea kuzingirwa na majeshi ya Russia na kumiminiwa mabomu. Zelemsky anatangaza kuwa waUkraine watapambania uhuru wao mpaka mwisho na watashinda pia.
Wote wawili (Al-Sahaf na Zelensky) wanaonekana kuwa na misimamo ya kutoyumbishwa na changamoto. Ingawa Zelensky yeye anajitutumua kwa Russia huku akiomba msaada kwa Marekani na NATO, wakati Al-Sahaf (Baghdad Bob) alikuwa akimkazia Marekani na akiwataka waIraq wawe na imani juu ya Saddam na jeshi la Iraq kuwa watamwangamiza na kumshinda adui (majeshi ya Marekani).
Chanzo cha habari hii ni: