Zembwela afunika kwenye Mkasi

Nakubaliana na wewe,
Zembwela toka tulipomchana hapa jf kuwa elimu ni ndogo
naona amepiga piga kitabu sana, hivyo kwa sasa mambo yake ni mswano kabisa,
hongera sana dogo zembwela.

kuna yule dogo wakumuita Baruti ana akili sana...amemshepu Zembwela mpaka sasa akiongea unasikia logic ndani yake..sina uhakika sana na shule zao ila Baruti ukimsikiliza hauitaji kuuliza kama kaenda shule.
 
marudio huwa lini maana sikuangalia mkuu
 
tid ndio aliye funika kwa ku boa. ila zembwela ki ukweli kafanya vizuri sana.ngoja tumngoje diamond wiki ijayo coz kwenywe tangazo kaulizwa kua mara ya mwisho kafanya mapenzi lini akasema jana.inamaana huyu dogo ni mnzinzi mwambo mwisho.wenzake wanatubu mwezi huu yeye ndo anajitangaza kwenye tv.
 
Na mimi nilipenda sana yale mahojiano, ila mimi kitu ambacho sikipendi kwenye kile kipindi, ni vijana wale John na Muba kuwa wanauliza maswali, sidhani kama wana ujuzi wa kuuliza maswali.
 
Daudi Mchambuzi ndugu yangu leo umepatikana...
Mie naogopa hata kuingilia
 
mkuu kuchanganya lugha ni makosa katika mawasiliano ya kawaida au mazungumzo ya mtu na mtu tofauti na mambo ya kiofisi au sehemu rasmi ni makosa mkuu?? hapa siwazungumzii wale wanaojifanya kama wanajua nazungumzia kwa mazingira ya kawaida tu maana hata mimi huwa najikuta nachanganya lugha hadi la kabila langu hapo nina makosa? funguka mkuu unisaidie kwa hili kama ni kosa kwa jamii.
 
kuna yule dogo wakumuita Baruti ana akili sana...amemshepu Zembwela mpaka sasa akiongea unasikia logic ndani yake..sina uhakika sana na shule zao ila Baruti ukimsikiliza hauitaji kuuliza kama kaenda shule.

Michael Baruti classmate wangu O_level......kichwa jamaa...ana degree ya uandishi habari...
 
Na mimi nilipenda sana yale mahojiano, ila mimi kitu ambacho sikipendi kwenye kile kipindi, ni vijana wale John na Muba kuwa wanauliza maswali, sidhani kama wana ujuzi wa kuuliza maswali.

Hasa yule dogo mwenye rasta kama Awilo Longomba ndio amejaa pumba tupu, naona anadhihirisha kwamba kichwa kina matumizi mengi.
 
Hata sitaangalia, sitaki kutapika mimi.
 
kumbe bongo hakuna Celeb enhee kuna masuper star
 
Kuchanganya lugha "code mixing" ni makosa ya kimazungumzo ambayo mara nyingi hutokea katika hali tofauti zifuatazo.
1. Makusudi - Kama mzungumzaji anataka kuonesha jinsi alivyo mlumbi lugha (mjuzi/ mweledi wa lugha mbalimbali)
2. Bahati mbaya - kama mzungumzaji anajaribu kuzungumza lugha ambayo bado hajaimudu vizuri.
3. Ulimbukeni - pale mtu anapodhani kuchanganya lugha ndio ujanja na unamletea heshima miongoni mwa wasikilizaji. Mf - msajili wa vyama.
Sasa wewe, uko kwenye kundi gani?!
 
ha ha ha ha ha mimi sipo kwenye hilo kundi hata mojawapo. ila unachoongea kinawezekana kuwa kweli na vile vile sio kweli inategemea na mtu na mazingira alikokulia.
 
Salama alipomwambia fresh, Zembwela akajibu mtindi! ilichekesha kwa kweli. tena yeye sio mnyama kwa kuwa mnyama huwa anadu na yeyote hata mzazi wake.
 
Hii interview nimeangalia leo nimecheka sana!
Mkasi unaweza kuangalia Youtube ukiimiss.
Salama naona hata hakuwa na maswali mengi maana jamaa aliwapeleka shule.
 
Daudi samahani km ntakukwaza ila naomba kuuliza we ni muhaya eeh.
 
ameamua kusema ukweli...kwani we mapenzi huwa hufanyi???...hoja za camerron zikipita utakua wa kwanza kuolewa mkuu
 
Niliangalia kupitia YouTube zebwela yupo makini... Yule kijana john aache kurukia maswali utakuta swali halijajibiwa yeye karukia lingine...
 
kuna yule dogo wakumuita Baruti ana akili sana...amemshepu Zembwela mpaka sasa akiongea unasikia logic ndani yake..sina uhakika sana na shule zao ila Baruti ukimsikiliza hauitaji kuuliza kama kaenda shule.

Baruti keshawatoka EATV!Kapata kazi mitaa yaposta kama sikosei!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…