Hii batch ndio wale wa darasa la saba 2005. Mwaka huo asilimia 62 (kama 400,000) kati ya watihaniwa 700,000 walifaulu. Kwahiyo mwaka huo kuna kama vijana 300,000 walioachwa nyuma (walifeli). Sasa basi, wale 400,000 waliofaulu na kuendelea na O level, ndio matokeo yao tumeyaona majuzi na kati yao wengine ndio wameachwa nyuma. Walioachwa ni 200,000 ambao wamepata daraja la 4 na 0. Ukijumlisha hawa wa kidato cha nne mwaka 2009, na wenzao kiumri ambao walifeli darasa la saba 2005, jumla tuna kama vijana laki 700,000 nchini kwa sasa ambao system ya elimu ya Tanzania imewashinda.
Hypothetically, tunaweza kusema kuna vijana kama Laki Saba wenye umri kati ya 16-19 ambao academically ni failures. This is easily 2% of Tanzania's population.
Sasa, kila mwaka tukiwa tunafelisha wanafunzi, baada ya miaka kumi nchi yetu itakuwa inazidi kuwa ni nchi ya wasio na elimu ya kutosha. Imagine tukiendelea na rate hii hii ya vijana kufeli mitihani, huko mbele tutapata kweli nguvu kazi ya kutusaidia kusonga?