Mtangazaji wa siku nyingi wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC, Bi Zeyana Seif amezikwa nchini Uingereza.Bi Zeyana aliaga dunia tarehe 29 Disemba 2008 mjini London.
Baada ya kuswaliwa katika msikiti mkuu ujulikanao kama East London Mosque huko Whitechapel, mwili wa Bi Zeyana ulipelekwa katika makaburi ya Gardens of Peace, Essex kwa mazishi - Jumamosi ya tarehe tatu 2009.
Miongoni mwa watu waliofika msikitini kumswalia Bi Zeyana ni ndugu, jamaa na marafiki kutoka sehemu mbali mbali duniani akiwemo balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Bi Mwanaidi Sinare Maajar.