Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
JULIUS NYERERE, ZUBERI MTEMVU NA BI. MAIDA SPRINGER ZANZIBAR 1957
Nimekutana na Bi. Maida Springer katika nyaraka za Sykes miaka mingi iliyopita
Leo nimepokea makala kutoka watu mbalimbali zote zikieleza hotuba ambayo Julius Nyerere alitoa Zanzibar tarehe 1 February 1957 akiwa ameongozana na Zuberi Mtemvu na Bi. Maida Springer.
Nyerere na ujumbe wake makala inaeleza walikuwa wageni wa African Association iliyokuwa ikiongozwa na Abeid Amani Karume.
Katiba hotuba hiyo aliyotoa usiku wa saa tatu Kisimama Majongoo Nyerere alisema, '' Sisi ni watu wawili tunataka kufyeka pori na pori hilo sharti tuwe na panga na bei ya panga ni shilingi tatu na sisi ni watu wawili kila mmoja ana shilingi moja.
Je ile shilingi ya tatu tutaipata wapi?
...sisi tunataka kufyeka mwitu huo tuwe sote mkono mmoja, tuungane tuchange tununuwe panga, ndipo tutapo weza kuweka safi huu mwitu, huu ni wakati wa kuwa pamoja.
Waafrika wasijiweke nyuma tena, kuna mambo mengi yanayoturejesha, hata majumba tuyakaayo sisi yanaonesha hali mbaya.
Hao wenzetu wa Amerika ni matajiri wa kweli, wazee wangu na ndugu zangu nawaambia tufanikiwe, mkifanikiwa nyinyi na sisi tutafanikiwa, tena hata sisi tukifuzu na nyinyi mtafuzu bila ya shaka.
Tuondoe hiki kizingiti cha upotovu tuwe sote sauti moja.''
...ndipo ilipo amuliwa kuunganisha chama cha Shirazi Association na African Association ili kuundwa Afro Shirazi Party (ASP)...''
Hii ilikuwa TANU mwaka wa 1957.
Huyu alikuwa Julius Nyerere mwaka wa 1957 viongozi wanakijenga chama Tanganyika na wakati huo huo kujaribu kuisaidia Zanzibar kuasisi chama.
Lakini Zanzibar kulikuwa na chama cha kupigania uhuru wa Zanzibar, Zanzibar Nationalist Party (ZNP).
Kwa nini Julius Nyerere alitaka kuwepo na chama kingine?
PICHA: Bi. Maida Springer.