Ziara ya Juliana Shonza Katika Kituo cha Afya cha Tunduma

Ziara ya Juliana Shonza Katika Kituo cha Afya cha Tunduma

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

Ziara ya Juliana Shonza Katika Kituo cha Afya cha Tunduma

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe, Mhe. Juliana Daniel Shonza ametembelea Kituo cha Afya Tunduma kwa lengo la kukagua mazingira ya utoaji huduma na kuwajulia hali wanawake waliojifungua pamoja na watoto wachanga waliozaliwa Katika Kituo cha Afya cha Tunduma.

Mhe. Juliana Shonza amefika katika Kituo cha Afya cha Tunduma akiwa na zawadi mbalimbali ambapo amepeleka Mashuka 30, Net 30, Pampas za Watoto, Madishi ya kufulia Nguo, Kanga, Sabuni za miche na sabuni za unga kwaajili ya watoto waliozaliwa kituoni hapo.

"Nimechagua kwenda kituo cha afya Tunduma sababu ya kuunga mkono kazi kubwa aliyofanya Mheshimiwa Rais toka akiwa Makamu wa Rais, wakati alipokuja kwenye Kampeni mwaka 2015 alikikuta ni Zahanati yenye changamoto nyingi huku kikihudumia watu zaidi ya laki moja. Alituahidi na mara baada ya kampeni alitekeleza na kuja kukuzindua yeye mwenyewe" - Mhe. Juliana Shonza.

Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati akiwa Makamu wa Rais kwenye Kampeni za uchaguzi wa mwaka 2015 aliahidi kufanya maboresho ya Zahanati kuwa Kituo cha Afya cha Tunduma ambapo fedha zilikuja na maboresho makubwa yamefanyika kwa kuongeza majengo mengi ya kisasa, Vifaa Tiba, Madaktari na Manesi ambapo kimekuwa kikijitosheleza.

Aidha, Mhe. Juliana Shonza ametumia nafasi hiyo kuelezea utekelezaji wa Ilani ya CCM 2020-2025 kwa miradi iliyofanyika ikiwemo mradi mkubwa wa Maji kutoka Mto Momba na kuyaleta Mji wa Tunduma, Vwawa na Mlowo. Mradi wa Maji upo kwenye bajeti na Mkandarasi ameshapatikana na utatekelezwa kwa Miaka miwili ambao utamaliza kabisa Changamoto ya Maji katika Mji wa Tunduma.

Vilevile, Shonza amesema kuwa Jimbo la Tunduma lenye Kata 14 lilikuwa na Zahanati moja tu na hapakuwa na Kituo cha Afya hata Kimoja lakini ndani ya Miaka mitatu ya Mama Samia Suluhu Hassan Tunduma imepata vituo vya afya Vitano ikiwemo Kituo cha Afya cha Chiwezi, Chapwa, Mwakakati, Mpande.

Shonza amesema, Wilaya ya Momba imepata Hospitali ya Halmashauri inayojengwa Mpemba yenye hadhi ya Hospitali ya Wilaya. Pia, ipo Hospitali ya Wilaya ya Momba inayojengwa Chitete yenye hadhi ya Hospitali ya Wilaya. Haya ni mafanikio makubwa sana na wanawake wa Tunduma wameendelea kumuahidi na kumhakikishia kumtafutia kura nyingi Mheshimiwa Rais usiku na mchana.

Juliana Shonza amesema kuwa Wanawake wa Mkoa wa Songwe wamekubaliana ifikapo mwaka 2025 wana jambo lao kwa kazi kubwa anayoifanya Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ndani ya Miaka mitatu ya uongozi katika Jimbo la Tunduma.

Mwisho, Mhe. Juliana Daniel Shonza amesema kuwa, Wananchi wa Jimbo la Tunduma wanatamani kumuona Mheshimiwa Rais na wanaomba aweze kufika ndani ya Mkoa wa Songwe ili aone fedha nyingi za miradi ya maendeleo namna ambavyo zimefanya kazi na kugusa Changamoto za wananchi na kubadilisha Mkoa wa Songwe ambao ni Mkoa wa kimkakati.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2024-05-13 at 18.30.12.jpeg
    WhatsApp Image 2024-05-13 at 18.30.12.jpeg
    86.2 KB · Views: 6
  • WhatsApp Image 2024-05-13 at 18.30.14.jpeg
    WhatsApp Image 2024-05-13 at 18.30.14.jpeg
    105.3 KB · Views: 5
  • WhatsApp Image 2024-05-13 at 18.30.16.jpeg
    WhatsApp Image 2024-05-13 at 18.30.16.jpeg
    157.8 KB · Views: 6
  • WhatsApp Image 2024-05-13 at 18.30.19.jpeg
    WhatsApp Image 2024-05-13 at 18.30.19.jpeg
    156.2 KB · Views: 7
  • WhatsApp Image 2024-05-13 at 18.30.20.jpeg
    WhatsApp Image 2024-05-13 at 18.30.20.jpeg
    156.7 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2024-05-13 at 18.30.21.jpeg
    WhatsApp Image 2024-05-13 at 18.30.21.jpeg
    117 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2024-05-13 at 18.30.24.jpeg
    WhatsApp Image 2024-05-13 at 18.30.24.jpeg
    131.4 KB · Views: 6
  • WhatsApp Image 2024-05-13 at 18.30.25.jpeg
    WhatsApp Image 2024-05-13 at 18.30.25.jpeg
    98.2 KB · Views: 8
  • WhatsApp Image 2024-05-13 at 18.30.27.jpeg
    WhatsApp Image 2024-05-13 at 18.30.27.jpeg
    126.1 KB · Views: 8
  • WhatsApp Image 2024-05-13 at 18.30.29.jpeg
    WhatsApp Image 2024-05-13 at 18.30.29.jpeg
    128.4 KB · Views: 8
  • WhatsApp Image 2024-05-13 at 18.30.30.jpeg
    WhatsApp Image 2024-05-13 at 18.30.30.jpeg
    81.8 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2024-05-13 at 18.30.34.jpeg
    WhatsApp Image 2024-05-13 at 18.30.34.jpeg
    100.3 KB · Views: 7
  • WhatsApp Image 2024-05-13 at 18.30.31.jpeg
    WhatsApp Image 2024-05-13 at 18.30.31.jpeg
    59.6 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2024-05-13 at 18.30.34.jpeg
    WhatsApp Image 2024-05-13 at 18.30.34.jpeg
    100.3 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2024-05-13 at 18.30.35.jpeg
    WhatsApp Image 2024-05-13 at 18.30.35.jpeg
    124 KB · Views: 5
Back
Top Bottom