Ziara ya Loyce Kwezi - Mbunge Jimbo la Kaliua, Tabora

Ziara ya Loyce Kwezi - Mbunge Jimbo la Kaliua, Tabora

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Mbunge wa Jimbo la kaliua Loyce Kwezi amendelea na ziara ya utatuzi wa kero za Wananchi Katika kijiji cha Kangeme Kata ya Zugimlole na amechangia shilingi milioni 5 kwa ajili ya upauaji wa Shule Shikizi. Akizungumza na Wananchi, Kwezi amewaeleza jinsi Serikali ya Awamu ya Sita Ilivyotoa fedha nyingi katika Jimbo la kaliua.

FqPh7zvWIBc-8_E.jpg

"Jimbo letu la Kalia kwa kipindi cha miaka miwili tumeletewa shilingi bilioni 60 za miradi ya maendeleo ndio maana tumejenga barabara za lami KM 11.5. wiki mbili zijazo tunafunga taa kutoka Relini mpaka Kasungu. Hata hivyo kwa miaka miwili tumejenga Sekondari 5 Kasungu, Mpandamlowoka, Ugansa, Dkt Magufuli, Kamsekwa na Usimba" - Mbunge Loyce Kwezi

"Hapa Kangeme nimekwisha kuja mara nyingi lakini kwa sasa nimekuja kivingine, tumebadirisha mitaa, kwa sasa tuko na Loyce Kwezi, zile changamoto zilizokuwa zinatukabili kwa zaidi ya miaka 15 huko nyuma sasa basi tumepata tumekuja sisi CCM na zao la CCM Kwezi na Balikeka" - Ndugu Msigwa Kalokaza, Katibu Kata Usinge.

FqPh8t2WIAgTh3J.jpg

"Sisi tunaoishi Kaliua tunayaona maendeleo na lazima tuyaseme kuwaeleza Wananchi mambo yanayofanywa na Diwani Balikeka na Loyce Kwezi Mbunge Jimbo la kaliua anatupambania sana na Rais wetu Suluhu Samia" - Ndugu Leah Boniface, Katibu Mwenezi Kata ya Kaliua.

"Tumepata Mbunge Mchapakazi Loyce Kwezi anasikiliza kero za watu, analeta maendeleo tunayaona kwa macho na mengi yamefanyika Kwa kipindi hiki kasi ya maendeleo kwa miaka miwili ya Kwezi ni kubwa sana tumunge mkono tushirikiane nae." - Ndugu Kabangaya, Katibu Mwenezi Kata ya Igalala.
FqPh86MWIAEjT7P.jpg

Wananchi wa Kijiji cha Kangeme Kata ya Zugimlole Wilaya ya Kaliua wamempa zawadi ya asali Mbunge wa Jimbo la Kaliua Loyce Kwezi baada ya kumaliza mkutano wake na wakazi hao.

#Kaziendelee
 

Attachments

  • FqPh7SHWIA47-hu.jpg
    FqPh7SHWIA47-hu.jpg
    291.6 KB · Views: 6
  • FqPh9AdWIBckAag.jpg
    FqPh9AdWIBckAag.jpg
    534.5 KB · Views: 3
Back
Top Bottom