Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kusini, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo Mhe. David Mwakiposa Kihenzile amefanya ziara ya siku saba kijiji kwa kijiji ikiwa ni utaratibu wake wa kukutana na wananchi wake kila Kijiji angalau mara moja kwa Mwaka.
Mhe. Kihenzile akiwa katika Kata ya Luhunga alikagua Barabara ya lami ya 30.4KM ya Agroconect ambayo ilizinduliwa na Rais wa JMT Mhe. Samia Suluhu Hassan mwezi Agosti 2018. Pia, alitembelea kipande kilichobaki cha Km 10.4 kinachounganisha Iyegea-Lulanda ambacho ujenzi wake utaanza hivi karibuni.
Mhe. Kihenzile alifanya Mikutano ya Hadhara na kutembelea Miradi kwenye Vijiji Vya Mtwango na Sawala-Mtwango na Itulituli&Kihanga-Mninga ikiwa ni utaratibu wake wa kukutana na wananchi wake kila Kijiji.
Aidha, Mhe. David Kihenzile aligawa bati zenye thamani ya Shilingi Milioni Tano kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa ofisi za CCM Wilayani Mufindi. Aligawa bati hizo katika ziara ya Februari 25, 2023 kwenye Kata ya Itandula.
Lengo la ziara ilikuwa ni kuzungumza na Wananchi, Kukagua Miradi ya Maendeleo na Shughuli za chama. Mhe. Kihenzile amesema bati 70 ni za Ofiisi ya Kata ya Itandula, Bati 50 za Ofisi ya CCM Tawi la Ikiliminzowo na Bati 30 za ujenzi wa ofisi ya Tawi la Ihawaga.
Mhe. Kihenzile amewaeleza wana Itandula dhamira ya Serikali ya CCM ilivyotenga fedha Sh. 168 Milioni kwa ajili ya kujenga Kituo cha Afya cha Kata. Fedha hiyo imetengwa katika bajeti ya kuanzia Julai 2023 huku Shilingi Milioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa Sekondari ya Vipaji Maalumu itayojengwa kwenye Kata hiyo.
Mhe. Kihenzile amepongeza Jitihada za Viongozi na wanaCCM Kata hiyo kwa kuanza ujenzi huo na akawaahidi kuendelea kuwaunga Mkono.
Mapema Mwaka 2023, Mhe. Kihenzile alifanya vikao na viongozi wa CCM wa Kata na Matawi na kuwasihi kila Kata kuwasilisha Mpango Kazi na vipaumbele vyake huku akiziomba Kata zote zisizo na Ofisi kuweka ujenzi huo Kipaumbele cha mwanzo.
Mbunge huyo alihitimisha ziara yake ya siku Saba ambapo alitembelea na kukutana na wananchi wa Kata za Luhunga, Mtwango, Mninga, Malangali na Itandula ikiwa ni kwenye utaratibu wake kufikia kila Kijiji kwa Mwaka.
Kwenye ziara hiyo ya Siku saba alikagua hali ya usambazaji wa Mbolea ya ruzuku kwa wananchi sambambamba na kufafanua mipango mikubwa ya Serikali ikiwemo kushukuru Serikali kwa ujenzi wa Kiwanda cha Parachichi na ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi VETA unaotarajiwa kuanza hivi karibuni Nyololo.
Pia Miradi mingi ya Maji pamoja na Ujenzi wa kiwango cha lami kwa barabara za Mafinga-Mgololo na Nyololo-Mtwango iliyokwishapitishwa kwenye bajeti ya 2022/2023 huku Tathminini ya kina ikiwa inatarajiwa kuanza kwa barabara za Nyololo-Kasanga- Nyigo na Mgololo-Makambako
Aidha, Mhe. Kihenzile amewaahidi wananchi wake anaendelea kuunga mkono shughuli za Chama na za wananchi kadri itakavyowezekana.