Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
ZIARA YA MBUNGE MAVUNDE YALETA MATUMAINI MAPYA KATA YA HOMBOLO MAKULU
- Kuanzisha ujenzi wa Zahanati Mtaa wa Maseya
- Shule Mpya kujengwa Kitongoji cha Mgona ngholongo
- Atoa vifaa vya ujenzi kukamilisha ujenzi wa ofisi za Mitaa
- Wananchi wamshukuru Rais Dkt. Samia S. Hassan kwa miradi ya mendeleo
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde jana amefanya ziara ya kukaguza shughuli za maendeleo na mikutano katika mitaa ya Msisi,Kangalima na Maseya Kata Ya Hombolo Makulu.
Katika mikutano hiyo Mbunge Mavunde alipata nafasi ya kusikiliza kero za wananchi na kuzipatia majibu;
1. UKOSEFU WA ZAHANATI
Tarehe 8.07.2024 Kuanza ujenzi wa Zahanati ya Maseya kwa nguvu za wananchi,wawekezaji na Mbunge.
2. UHITAJI WA SHULE MPYA YA MSINGI
Ujenzi wa jengo la Darasa kuanzisha Shule ya Msingi Mpya ya Mgona Ngh’olongo.
3. UMALIZIAJI WA OFISI ZA MITAA
Mchango wa Vifaa vya Ujenzi vyenye thamani ya Tsh 6,000,000 kumalizia ujenzi wa Ofisi za Mitaa ya Kangalima,Maseya na Msisi.
Wakizungumza katika mikutano hiyo Diwani wa kata ya Hombolo Makulu Mh. Gideon Nkana na Diwani wa Kata ya Hombolo Bwawani Mh. Assed Ndajilo wameishukuru na kupongeza serikali ya awamu ya sita chini ya Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan kwa miradi mikubwa ya maendeleo ambayo inaleng kuboresha huduma za kijamii sambamba na ujenzi wa daraja kubwa linalounganisha kata hizo mbili.
Attachments
-
WhatsApp Image 2024-06-30 at 19.17.41.jpeg169.3 KB · Views: 5 -
WhatsApp Image 2024-06-30 at 19.17.41(1).jpeg135.3 KB · Views: 5 -
WhatsApp Image 2024-06-30 at 19.17.41(2).jpeg127.1 KB · Views: 6 -
WhatsApp Image 2024-06-30 at 19.17.42.jpeg86.7 KB · Views: 5 -
WhatsApp Image 2024-06-30 at 19.17.42(1).jpeg214.8 KB · Views: 5 -
WhatsApp Image 2024-06-30 at 19.17.43.jpeg77.2 KB · Views: 6 -
WhatsApp Image 2024-06-30 at 19.17.43(1).jpeg139.1 KB · Views: 6 -
WhatsApp Image 2024-06-30 at 19.17.43(2).jpeg121.3 KB · Views: 9 -
WhatsApp Image 2024-06-30 at 19.17.44.jpeg123 KB · Views: 5 -
WhatsApp Image 2024-06-30 at 19.17.44(1).jpeg163.5 KB · Views: 4 -
WhatsApp Image 2024-06-30 at 19.17.45.jpeg195.3 KB · Views: 4