Ziara ya Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Juliana Shonza kata ya Hasanga wilayani Mbozi - Songwe

Ziara ya Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Juliana Shonza kata ya Hasanga wilayani Mbozi - Songwe

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

ZIARA YA MHE. SHONZA KATA YA HASANGA WILAYANI MBOZI - SONGWE

Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Songwe Mhe. Juliana Danieli Shonza ameendelea na ziara yake katika maeneo mbalimbali ya Mkoa na Songwe ikiwa na lengo kushirikiana na wananchi hususani wanawake katika ujenzi wa kituo cha Afya kinachojengwa kwa nguvu ya wananchi. Katika ziara hiyo Mhe. Shonza amefanya yafuatayo;

1. Amechangia Matofali 3000
2. Amenunua Chakula na kuwapikia Mafundi na Wananchi walioshiriki katika ujenzi siku hiyo
3. Aliongoza zoezi la kugawa Miche ya Miti 1200 katika taasisi mbalimbali za Kidini, Kielimu, Kichama pamoja na kuendesha zoezi la kupanda miti kwenye kituo cha Afya kinachojengwa.

Baada ya hapo Mhe. Shonza alipata wasaa wakuongea na wananchi katika Kata hiyo kuelezea utekelezaji wa ilani ya Chama Cha mapinduzi (CCM) chini ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan. Katika kipindi chake cha miaka miwili, Kata hiyo imeshapokea Shilingi Milioni 250 kwaajili ya miradi mbalimbali ya kimaendeleo.
Mhe. Shonza aliwapongeza wananchi kwa jitihada walizofanya kwa kuunga mkono jitihada za serikali na kuawaahidi yeye kama Mbunge anaenda kusimamia bungeni kuhakikisha Serikali inakamilisha boma hilo kwa kuwapatia Shilingi Milioni 500 za umaliziaji wa jengo, Vifaa tiba hasa wodi ya wanawake na watoto, Madaktari na Manesi wakutosha.

Mhe. Shonza amezungumzia umuhimu wa malezi kwa Watoto wote, kila mzazi awe anawajibika kulea na kufatilia makuzi ya watoto kutokana na janga la mmomonyoko wa maadili ubakaji na ulawiti. Pia, Suala la lishe bora kwa watoto ambayo ni changamoto kubwa kwa watoto, Songwe ni miongoni mwa mikoa yenye tatizo la udumavu Tanzania, na kwamba serikali iko mbioni kuandaa mwongozo wa lishe kwa watoto ili kuepusha kila mtu kujitengenezea unga wa lishe vile anavyotaka.

Mhe. Shonza amezungumzia Suala la mbolea na ammemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa Ruzuku ya Shilingi Bilioni 150 na kuwaahidi wananchi kwamba changamoto zilizojitokeza katika zoezi hili ikiwepo uchepushaji wa mbolea unaofanywa na wafanyabiashara wasio waaminifu pamoja na uhaba wa vituo vya kuuzia mbolea, Serikali itazifanyia kazi katika msimu ujao nakwamba hazitajitokeza tena.

Tayari Mkuu wa wilaya ya Mbozi ameshawakamata wafanyabiashara wanaohusika na uchepushaji wa mbolea na kuziuza kwa bei kubwa. Mhe. Shonza amewaeleza kuwa wao kama wabunge wameishauri Serikali kuwe na vituo vingi vya kuuzia mbolea angalau kila Kata ili wananchi wasihangaike kufuata Mbolea mbali hali inayopelekea rushwa katika uuzaji wa Mbolea.

WhatsApp Image 2023-02-22 at 18.08.28.jpeg

WhatsApp Image 2023-02-22 at 18.08.22.jpeg

WhatsApp Image 2023-02-22 at 18.08.19.jpeg

WhatsApp Image 2023-02-22 at 18.08.16.jpeg

WhatsApp Image 2023-02-22 at 18.08.18(2).jpeg
 
Back
Top Bottom