Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo na Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amehitimisha ziara ya Kiserikali katika kata 21 za Manispaa hiyo ambapo amezungumza na kutatua kero mbalimbali za wananchi wa kata hizo.
Miongoni mwa kero zilizowasilishwa na wananchi hao katika ziara hiyo ni ubovu wa miundombinu ya barabara (madaraja na vivuko), ukosefu wa huduma ya maji safi na salama kwa baadhi ya maeneo, uchakavu wa vyumba vya madarasa pamoja na usambazaji wa huduma ya umeme ambazo zilipokelewa na Serikali kupitia jopo la wataalam walioambatana na kiongozi huyo walitoa ufafanuzi na kueleza mipango ya kukabiliana na changamoto hizo ili kuzimaliza kabisa.
Aidha, kuhusu kero ya ukosefu wa huduma ya maji katika baadhi ya maeneo ya Manispaa hiyo, Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Manispaa ya Songea (SOUWASA) kupitia Muhandisi wake Laurent Pasekana imeweka wazi juu ya mwarobaini wa kero hiyo kwa kuanza utekelezaji wa mradi mkubwa Serikali wa maji katika miji 28 ambao utekelezaji wake umeshaanza na Mkandarasi yupo eneo la kazi na kazi hiyo inaendelea.