Spika wa Baraza la Wawakilishi la Bunge la Marekani Nancy Pelosi hivi karibuni alifanya ziara Taiwan, China, na kuongeza hali ya wasiwasi ya kikanda na ya kimataifa. Kitendo hiki cha kisiasa kinacholeta hasara kwa pande zote kimeonyesha kuwa, mfumo wa kisiasa wa Marekani ni kama mgonjwa.
Kwanza kabisa, ziara ya Pelosi katika sehemu ya Taiwan imeiumiza China. Suala la Taiwan ni moja ya maslahi makuu ya China. Nchi 181 duniani zimeanzisha uhusiano wa kidiplomasia na China kwa kufuata kanuni ya kuwepo kwa China moja, ambayo inaonyesha kuwa kanuni hiyo ni makubaliano ya pamoja ya jumuiya ya kimataifa. Akiwa kiongozi namba tatu wa serikali ya Marekani, Pelosi amekiuka kanuni hiyo kwa kutembelea Taiwan bila ya kujali kupingwa vikali na China. Kitendo chake kimeharibu mamlaka na ukamilifu wa ardhi ya China, na kuumiza uhusiano wa China na Marekani na hisia za watu wa China.
Ziara hiyo pia imedhuru zaidi maslahi ya Taiwan. Baadhi ya watumiaji wa mtandao wa Taiwan wamesema kuwa, Pelosi amecheza na moto bila kujali usalama wa watu milioni 23 wa Taiwan. Taiwan ni sehemu isiyotengeka ya China, lakini sasa Marekani inaitumia kama silaha ya kuzuia maendeleo ya China. Ziara ya Pelosi imezidisha mvutano kati ya pande hizo mbili katika suala la Taiwan, na kuongeza uwezekano wa kutokea kwa migogoro katika mlangobahari wa Taiwan.
Ziara ya Pelosi katika sehemu ya Taiwan pia inakwenda kinyume na maslahi ya Marekani. Hivi sasa Marekani inakabiliwa na mfumuko wa bei uliokuwa mbaya zaidi tangu mingo kadhaa iliyopita, na mzozo wa Russia na Ukraine. Licha ya hitaji la kushirikiana na China ili kukabiliana na changamoto hizo, kuikasirisha China na kuzusha migogoro mipya bila shaka hakulingani maslahi ya Marekani.
Tukitafuta manufaa ya zaira hiyo, labda ni kwake yeye tu binafsi. Lengo la wazi la ziara ya Pelosi katika sehemu ya Taiwan ni kuharibu maslahi makuu ya China, ili kuongeza uwekezano wa ushindi kwa Chama chake cha Kidemokrasia kwenye uchaguzi utakaofanyika miezi mitatu ijayo. Lakini ukweli ni kwamba, Pelosi anazingatia zaidi maslahi yake binafsi na ya kisiasa. Licha ya hayo, mbunge wa Marekani Marjorie Green alidokeza kuwa, safari ya Pelosi katika Taiwan haswa ni kwa ajili ya kumsaidia mume wake kufanya uwekezaji katika sekta ya Chips. Hata hivyo, mchezo huu wa kisiasa ambao kwa hakika utaleta hasara kwa pande zote zinazohusika hatimaye umefanyika, hali ambayo inathibitisha kuwa mfumo wa kisiasa wa Marekani ni kama mgonjwa.
Kabla ya safari ya Pelosi, mkurugenzi wa Shirika la Ujasusi la Marekani, Mwenyekiti wa Mkutano wa Viongozi Waandamizi, na timu nzima ya usalama wa taifa nchini Marekani walitoa pingamizi kwa pamoja. Ingawa Rais Joe Biden wa Marekani hakutoa tamko la wazi, lakini alinukuu maoni ya jeshi, kwamba Pelosi kutembelea Taiwan si wazo nzuri. Jambo la kushangaza ni kwamba kutokana na mfumo wa kisiasa wa Marekani, hakuna nguvu yoyote iliyomzuia Pelosi.
Kama kiongozi wa ustaarabu wa kisiasa wa Magharibi, Marekani inajivunia sana na mfumo wake wa kisiasa. Lakini katika miaka ya hivi karibuni, kutoka kwa ghasia za Capitol Hill, hadi kukwama kwa sera ya kudhibiti bunduki, na kisha ziara hiyo ya Pelosi kwenda Taiwan, mambo hayo yote yanaonesha kuwa mfumo wa kisiasa wa Marekani umekumbwa na shida na haufanyi kazi vizuri, na sasa ni wakati wa kuutiba kama mgonjwa.