Ruge Opinion
JF-Expert Member
- Mar 22, 2006
- 1,838
- 705
Hii siyo ziara. Kutoka ofisi yake Ikulu kwenda Hazina ni kama mita 300 hivi. Kwenda TRA/Long Room ni kama nusu kilometa. Hata bila yeye kwenda huko angeweza kuwaita wahusika wakaenda ofisini kwake na taarifa alizozitaka. Ni zuga zake za kila siku.Kumbe anakumbuka kufanya ziara nchini?? mi nilifikiri yupo Ughaibuni anakula gud tym.
Big up Kikwete kwa kuanza kufanya ziara nchini!
JK anaonekana kama anapata nuru ya usoni, haya ni matokeo ya KIKOMBE CHA BABU loliondo.
Mapato ya taifa yameongezeka kwa shilingi bilioni 205 tangu mwaka 2005 alipochanguliwa kuongoza taifa la Tanzania. Miaka ya nyuma mapato yaliyokuwa yanakusanywa ya shilingi bilioni 215 kwa mwezi yaliwezesha kujenga miradi mingi ya maendeleo iliyofadhiliwa na mapato yetu ya ndani na miradi imejengwa kwa ufanisi mkubwa.
Inakuwaje mapato yaongezeke mara mbili kisha miradi mingi ya maendeleo isimame? na hakuna mradi mwingine wowote mpya ambao umeanzishwa na serikali yake anaoweza kujivunia.
Tunataka jibu, pesa zetu zinapelekwa wapi?
Jk ni mchumi, sasa anaposema watafute njia za kupunguza inflation, anazungumza kwa nadharia, nilitegemea angetumia uchumi wake kushauri njia ipi itumike kupunguza inflation rate lakin jamaa yetu anatoa matumain mahali panapohitaji kutenda. Wakati huu si muda wakupeana matumaini alisha toa matumaini 5yrs ago hakuna alichotimiza aache ukilaza afanye maamuzi magumu.