Ziara ya Rais Putin nchini Korea Kaskazini imejaa mengi

Ziara ya Rais Putin nchini Korea Kaskazini imejaa mengi

HERY HERNHO

Senior Member
Joined
Mar 4, 2022
Posts
110
Reaction score
458
Rais wa Shirikisho la Urusi Putin amefanya ziara yake ya kwanza Korea Kaskazini katika kipindi cha miaka 24 iliyopita akiahidi kuimarisha uhusiano wa kibiashara na kiusalama na taifa hilo lililotengwa lenye silaha za nyuklia na kuliunga mkono dhidi ya Marekani.

Mkutano kati ya viongozi hao wawili unaonyesha “kutoshindwa na kudumu” kwa urafiki kati ya Korea Kaskazini na Russia, kulingana na shirika la habari la serikali ya Korea Kaskazini(KCNA).

Uhusiano wa Korea Kaskazini na Russia umeimarika “kama ngome imara ya kimkakati kwa kulinda sheria ya kimataifa, amani na usalama na kichocheo kwa kuharakakisha ujenzi wa ulimwengu wenye misimamo tofauti,” KCNA limesema.

Putin alitua katika mji mkuu wa Korea Kaskazini Pyongyang kabla ya alfajiri siku ya Jumatano ambapo Kim alikuwa akimsubiri kumsalimia licha ya saa za mapema.

Wanaume hao wawili walipeana mikono na kukumbatiana huku mwanamke aliyevalia hanbok ya kitamaduni ya Kikorea akimkabidhi Putin shada la maua mekundu.

Kisha Kim alijiunga na Putin katika gari lake la limozini waliposafiri pamoja katika msafara wa magari, kando ya barabara zilizopambwa kwa bendera ya Urusi na picha za kiongozi huyo wa Urusi, hadi kwenye Jumba la Wageni la Kumsusan (Kumsusan State Guest House)

Baadaye Putin na Kim walionyeshwa katika sherehe rasmi ya kuwakaribisha Kim Il Sung Square, huku safu za wanajeshi zikiwa zimesimama kwa umakini na umati wa watoto wakiwa wamejipanga kwenye uwanja huo ambao ulikuwa umepambwa kwa mabango na puto.

Hapo awali, shirika la habari la serikali ya Korea Kaskazini KCNA, lilielezea mkutano wa viongozi hao wawili kuwa tukio la kihistoria ambalo lilionyesha "kutoshindwa na kudumu" kwa urafiki na umoja kati ya Korea Kaskazini na Urusi.

Uhusiano wa nchi hizo mbili "umeibuka kama ngome imara ya kimkakati ya kulinda haki ya kimataifa, amani na usalama na injini ya kuharakisha ujenzi wa ulimwengu mpya
(new multi-polar world”)

Putin ameandamana na viongozi kadhaa wakuu, akiwemo Waziri wa Ulinzi Andrei Belousov, Waziri wa Mambo ya Nje Sergey Lavrov na Naibu Waziri Mkuu Denis Mantrurov.

Mshauri wake wa sera za kigeni, Yuri Ushakov, alisema hati kadhaa zitatiwa saini katika ziara hiyo, ikiwezekana ikiwa ni pamoja na makubaliano ya ushirikiano wa kimkakati wa kina.

Ziara hiyo inajumuisha tamasha la gala, mapokezi ya serikali na uwekaji wa shada la maua kwenye Mnara wa Ukombozi, wakfu kwa wanajeshi wa Jeshi Nyekundu waliosaidia kuikomboa Korea wakati wa Vita vya Kidunia vya pili, kulingana na shirika la hanari la RIA.

Korea Kaskazini imekuwa chini ya vikwazo vikali vya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa miaka mingi kutokana na mpango wake wa kutengeneza silaha za nyuklia na makombora. Urusi pia inakabiliana na vikwazo vya Marekani na washirika wake kuhusu uvamizi wa Ukraine.

Pamoja na China, mshirika mkuu wa Korea Kaskazini, Urusi imezuia mara kwa mara juhudi zinazoongozwa na Marekani za kuweka vikwazo vipya vya Umoja wa Mataifa kuhusu majaribio ya silaha za Korea Kaskazini na kurusha satelaiti.

Mnamo Machi, kura ya turufu ya Urusi ilimaliza ufuatiliaji wa vikwazo vya Umoja wa Mataifa, na kusababisha shutuma za Magharibi kwamba Moscow ilikuwa inataka kuepusha kuchunguzwa kwani inanunua silaha kutoka Pyongyang kwa matumizi nchini Ukraine.

Maafisa wa Marekani na Korea Kusini wamesema wanajadili chaguzi za utaratibu mpya wa kuifuatilia Pyongyang.

tazama hapa ilivyofana
View: https://youtu.be/alS3sPml1AE

Putin ambaye anafanya ziara yake ya kwanza Korea Kaskazini katika kipindi cha miaka 24, ameeleza katika taarifa iliyochapishwa kwenye vyombo vya habari vya serikali saa chache kabla ya kuwasili kwake, kuwa anashukuru uungaji mkono wa Korea Kaskazini kwa oparesheni maalumu ya kijeshi ya Russia ndani ya ardhi ya Ukraine.
 

Attachments

  • gettyimages-2157653203.jpg
    gettyimages-2157653203.jpg
    139.8 KB · Views: 17
Ujuaji wa Marekani ndio umepelekea muungano wa nchi zilizowekewa vikwazo.

Kuna mipango mingine miovu ukipanga mara nyingi hua inarudi kukudhuru wewe mwenyewe.

Marekani ilipanga mipango miovu dhidi ya Urusi,china,Korea kaskazini,Iran na Cuba.

Ilifanya Kila Hila ili nchi hizi zisizokubaliana na mawazo ya Marekani zitengwe,lakini matokeo yake zinaenda kuungana.

Muungano wa nchi hizi ni balaa kubwa kwa Marekani.

Hebu fikiria kirahisi TU,vipi nchi za Urusi, china, Iran na Korea kaskazini zikaanzisha umoja wa kijeshi Hali itakuaje?
Chokochoko nyingi za Marekani mwisho kachokonoa balaa.

Yaani alichokua anakikataa siku nyingi Sasa kimekuja.
 
"Gari aina ya limozini"Limousine si gari ya mabeberu hii,nilitegemea Korea kaskazini awe na kampuni yake ya magari na sio kutumia gari za mabeberu
 
Ujuaji wa Marekani ndio umepelekea muungano wa nchi zilizowekewa vikwazo.
Kuna mipango mingine miovu ukipanga mara nyingi hua inarudi kukudhuru wewe mwenyewe.
Marekani ilipanga mipango miovu dhidi ya Urusi,china,Korea kaskazini,Iran na Cuba.
Ilifanya Kila Hila ili nchi hizi zisizokubaliana na mawazo ya Marekani zitengwe,lakini matokeo yake zinaenda kuungana.
Muungano wa nchi hizi ni balaa kubwa kwa Marekani.
Hebu fikiria kirahisi TU,vipi nchi za Urusi, china,Iran na Korea kaskazini zikaanzisha umoja wa kijeshi Hali itakuaje?
Chokochoko nyingi za Marekani mwisho kachokonoa balaa.
Yaani alichokua anakikataa siku nyingi Sasa kimekuja.
Wanaungana alafu wanategemea soko ulaya na mataifa ambayo ni hasimu wao
 
"Gari aina ya limozini"Limousine si gari ya mabeberu hii,nilitegemea Korea kaskazini awe na kampuni yake ya magari na sio kutumia gari za mabeberu

Limousine : a large, luxurious car, especially one driven by a chauffeur who is separated from the passengers by a partition.
 
Uchokozi wa mabeberu kupitia ukraine umewacost sana mpaka sasa nadhani wanajutia kilichobaki wanaamua wapigane kufa na kupona kunusuru maslahi yao. Mfaransa anatimuliwa afrika, matumizi ya Dola yanapungua, maadui zao wanazidi kuwa na umoja. Ukraine kwenyewe kumekuwa kugumu. Mpaka nahisi kama Hali itaendelea hivi matumizi ya silaha za nuclear wanaweza anza kuzitumia Hawa mabeberu
 
Ni wahuni kama Russia na Isis na Alqaida na Islamic jihad na Alshabab na boko haram na Houthi na bila kusahau Hamas
 
Back
Top Bottom