Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Kuna watu maarufu ambao wamewahi kutembelea Tanzania, na kwa namna moja au nyingine kuwa chachu ya mwamko wa kisiasa nchini. Tumetembelewa na watu kama Fidel Castro, Che Guevara, Nelson Mandela, nk. Hata kama hawakuongea mengi wakiwa nchini, kuwapo kwao nchini kulileta hamasa na mwamko fulani ndani ya mioyo ya Watanzania juu ya kuwa na utawala wa haki na kuchukia utawala wa kifisadi usiojali kupoteza rasilimali za taifa na kuiweka nchi katika ukoloni mamboleo, mambo waliyoyapinga vikali.
Tanzania kwa sasa inazidi kuwa kinara wa utawala wa kifisadi unaokumbatia wageni na kuwajali zaidi ya wananchi katika nchi yao wenyewe. Sasa je, ziara ya Captain Ibrahimu Traole hapa Tanzania, italeta mwamko na msisimko wa kukataa utawala wa namna hiyo kwa Watanzania, kutia ndani na ndugu zetu wa JWTZ?