Yoyo Zhou
Senior Member
- Jun 16, 2020
- 126
- 215
Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi wiki iliyopita alifanya ziara ya siku saba katika nchi nne za Afrika, ambazo ni Namibia, Jamhuri ya Kongo, Chad na Nigeria.
Ziara hiyo inadumisha mwendelezo wa desturi ya mawaziri wa Mambo ya Nje wa China kufanya ziara ya kwanza ya mwaka nje ya nchi katika bara la Afrika, na imedumu kwa mikaka 35 tangu mwaka 1991. Ziara hii ina umuhimu mkubwa sana kwa kuwa inaonyesha ahadi endelevu ya China ya urafiki huu mkubwa unaobadilika kuendana na wakati na maendeleo ya Dunia ya Kusini, na kuwezesha utekelezaji wa matokeo ya Mkutano wa Kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC), kuimarisha ushirikiano wa kina katika Nyanja mbalimbali, na kuboresha maendeleo endelevu ya kina ya uhusiano wa China na Afrika katika mwaka huu wa 2025.
Maingiliano kati ya China na Afrika yanawakilisha mpango wa muda mrefu wa China kwa maendeleo na ustawi wa Dunia ya Kusini na pia ushirikiano wa kiuchumi na kidiplomasia wa kuvuka mpaka. China na Afrika zote zinatambua umuhimu wa kufanya uratibu katika maeneo ya amani na usalama, maingiliano ya kiuchumi ndani ya bara la Afrika, utulivu wa mnyororo wa ugavi, na ustawi wa kuvuka mpaka wa mabara ya Asia na Afrika. Historia hii ya ushirikiano kati ya pande hizo mbili inaunda msingi wa kupanua zaidi uhusiano wao wa kidiplomasia na kimkakati.
Uhusiano kati ya China na Afrika umeonyesha mafanikio makubwa katika mwaka 2024, ikiwemo uungaji mkono usioyumba na endelevu wa China kwa Afrika katika kutafuta njia ya usasa inayoendana na mazingira ya nchi husika, kuunda mfumo wa ushirikiano kama Mpango Kazi wa Beijing (2025-2027) uliofikiwa wakati wa Mkutano wa Kilele wa FOCAC uliofanyika Beijing, ushirikiano wa kiuchumi chini ya Pendekezo la Ukanda mmoja, Njia Moja (BRI), mabadilishano ya ngazi ya juu, ukuaji mkubwa wa ubora wa biashara, na ushirikiano wa pande nyingi wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Wakati China inaendelea kuwa mwenzi mkubwa wa kibiashara wa Afrika kwa miaka 15 mfululizo, matoke mazuri yamepatikana kupitia uratibu katika uhamishaji wa teknolojia, kuendeleza vipaji na ujenzi wa uwezo katika sekta mbalimbali ikiwemo utengenezaji, ugavi, miundombinu, dawa, uchumi wa kidijitali na kilimo.
Kupitia ziara ya Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi mwaka huu, matarajio ya mwaka 2025 yanaonekana kuwa tulivu na yenye ustawi, kuanzia kukabiliana kwa pamoja na changamoto ili kuendeleza ukuaji wa pamoja. Mkakati wa Afrika wa kutimiza Malengo ya Maendeleo ya Umoja wa Mataifa ya mwaka 2030 unaelekea kupata matokeo mazui kutokana na ushirikiano kati ya nchi za bara hilo na China, huku uhusiano wa kunufaishana na mifumo ya ushirikiano wa pande nyingi ikichukua nafasi kubwa katika kutimiza lengo hilo.
Pia, sera ya China ya kufungua mlango zaidi ni muhimu sana kwa biashara na ustawi wa Dunia ya Kusini kwa kuwa inapunguza ukosefu wa uwiano wa biashara na kuunga mkono biashara huria duniani, utandawazi wa kiuchumi na mgawanyo wa kazi. Kwa mfano, kutokana na kuanzishwa kwa ‘ushoroba wa kijani,’ sasa kuna fursa zaidi kwa bidhaa za kilimo kutoka nchi za Afrika kuingia katika soko kubwa la China.
Kujenga maingiliano yenye nguvu kunajumuisha mambo mengi zaidi ya biashara ma auratibu katika sekta za kilimo na nishati, kwani kunajumuisha pia kuzitambulisha China na Afrika kama washiriki katika mfumo mpana wa kimataifa.
Mwaka 2025, pande hizo mbili zinapaswa kuanza kujenga mwelekeo mpya ambao msingi wake ni ushirikiano, wa pande nyingi, mshikamano wa mabara, ujenzi wa amani ya dunia na maendeleo endelevu kwa kuimarisha ushirikiano kati ya pande hizo.
Ziara hii ya Waziri Wang Yi mwanzoni mwa mwaka, inaashiria mwanzo mpya wa mambo haya.