Ziara za kushtukiza

Ziara za kushtukiza

Bishop Hiluka

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2011
Posts
7,147
Reaction score
14,699
Kwa kuwa staili ya serikali yetu ni kufanya ziara za kushtukiza jamaa mmoja hivi karibuni naye aliamua kutekeleza kwa vitendo staili ya serikali pale alipopanga kufanya ziara kadhaa za kushtukiza katika sehemu mbalimbali zinazomuhusu.

Akaona aanze na ziara ya kushtukiza pale shuleni kwa mwanawe, maana kila siku anakunywa chai na kuondoka na daftari zake na yeye hajawahi kwenda shuleni kwao toka alipomuandikisha shule mwezi Januari.

Alifika shuleni na kumuona mwalimu mkuu, ambaye alianza kutetemeka alipoambiwa na huyu jamaa kuwa amekuja pale kwa ziara ya kushtukiza, sijui mwalimu alidhani ni mmoja wa Mawaziri wapya, maana jasho lilikuwa linamtiririka ghafla.

Akamkaribisha jamaa ofisini kwake na kuita walimu wote na kumtambulisha jamaa kuwa ni kiongozi amekuja kwenye ziara ya kushtukiza. Jamaa alipojitambulisha kuwa ni mzazi, walimu wote waanza kupumua kwa raha. Akawaambia kuwa ana mwanafunzi pale na amekuja ziara ya kushtukiza kujua maendeleo yake.

Baada ya mwalimu mkuu kusaka jina la mtoto akamwambia yule jamaa, “Mzee huyu mtoto hajaja shule mwezi wa tatu sasa, tulijaribu kukutafuta ikashindikana, hatujui yu wapi.”

Jasho likaanza kumtoka jamaa, yule mtoto kila asubuhi anampa nauli anaenda shule, na mara nyingi anamuomba michango kumbe hata shule haji.

Aliondoka bila kuaga presha ikiwa juu. Akaona aende kwenye genge la mke wake naye akamfanyie ziara ya ghafla amhadithie mambo ya mwanaye, alipofika pale akakuta kuna mdada mwingine anauza genge. Akamsalimu, na kumuuliza mwenye genge atampataje, jibu lake karibu lingemuua jamaa kama asingekuwa mkakamavu, “Mume wake kaja kumchukua na gari wameenda kununua shamba Bagamoyo”.

Akaondoka akiwa amechanganyikiwa, akajua hapa dawa yake ni moja tu, nayo ni Sabrina, mtoto wa Kinyaturu pale ambapo akipata maudhi huwa anaenda kubembelezwa. Akatwanga mguu kwa Sabrina naye akamfanyie ziara ya ghafla ili aupoze moyo wake.

Alipogonga mlango wa chumba chake akatoka mbaba wa miraba minne, “Karibu kaka, unasemaje?”

Jibu likamtoka huyo jamaa, “Samahani, miye nilimkopesha huyu dada wa chumba hiki vitenge, nilikuja kuuliza kama ameshapata hela yangu”.

Ama kweli ziara za kushtukiza zinataka moyo wa chuma jamani…
 
Nimetabasamu.
 
Back
Top Bottom