Serikali hii fake sasa imekuwa kama dalali wa madini tu. Hizi nchi zinataka madini tu. Yaani kwa ujinga Watanzania tunachukuliwa ardhi yetu wanapewa Urusi eti walime! Kwani Watanzania hawawezi kulima?
Sasa eti Singapore nayo ipewe mashamba ya kulima! Tunaenda wapi
Sasa huyu Mama badala ya kutatua matatizo ya wananchi amekuwa mwigizaji
Soma
Ziara ya Rais Samia Russia: Tanzania itapata nini katikati ya mashinikizo ya EU, Marekani?
Gentleman,
kwanza kabisa ni muhimu kufahamu kwamba,
haipo serikali duniani isiyochangamana na mataifa mengine ya ulimwengu kwa faida. Serikali zote duniani huchangamana kwa maslahi mapana ya wananchi wa pande zote husika kijamii, kisiasa na kiuchumi.
Miongoni mwa faida za mataifa ya ulimwengu kuchangamana ni pamoja na kutangaziana na kukuza fursa za uwekezaji, ajira, utalii, biashara, kilimo, elimu, uchimbaji, usafirishaji n.k
Na ndio maana unaona kuna mikataba mbalimbali ya kijamii, kisiasa na kiuchumi husainiwa baina ya wakuu wa nchi husika.
So,
gentleman,
tija za ziara za wakuu wa nchi nje ya nchi zao ni kubwa mno, na zina maslahi makubwa na mapana sana ya kijamii, kisiasa na kiuchumi kwa wananchi wa pande husika.
ila ukiwa na chuki binafsi moyoni, mihemko ikikubana sana, na ukiwa umeathirika zaidi na maamuzi yako mbalimbali yasiyo na tija kama vile, kufuata mkumbo baada ya kubebwa ufala wa kifikra na wajanja, kamwe huwezi kuana tija ya jambo hilo zito na muhimu sana kwa mataifa ya ulimwengu.
Pole sana gentlkeman, ikiwa unapitia hali hiyo