SoC03 Ziba pengo katika mawasiliano

SoC03 Ziba pengo katika mawasiliano

Stories of Change - 2023 Competition

DDAVYX

New Member
Joined
Sep 3, 2022
Posts
2
Reaction score
1
Katika kutafuta huduma mbalimbali toka sehemu tofauti-tofauti, Lugha ni nyenzo muhimu sana. Ili uweze kueleweka unachotaka, ni lazima utumie lugha inayoeleweka kwa atakaye kuhudumia. Mfanyo, mgonjwa anatakiwa kutoa maelezo kiasi Fulani kabla ya daktari kuagiza aina ya vipimo vitakavyomsaidia kugundulika kwa tatizo kwenye mwili wa mteja wake.

Katika andiko langu, nitajikita kwenye huduma kwa watu wenye matatizo ya Kusikia na kuongea (Bubu na kiziwi).

Siku moja nikiwa kwenye kituo Fulani cha kutolea huduma za afya, alifika mtu mmoja mwenye tatizo la kusikia na kuongea. Ni mgonjwa aliyetaka kupata huduma za afya. Ilikuwa ngumu sana kwa watoa huduma kuwasiliana naye kiasi kwamba hata ubora wa huduma aliyoipata bila shaka haikuwa na ubora kama kusingelikuwa na pengo katika mawasiliano baina ya pande hizi mbili. Alitumia lugha ya alama kutoa maelezo.

Maswali niliyojiuliza ni kama ifuatavyo,

Ni wangapi wanaokwama kupata huduma kamili katika taasisi wanazozitembelea?

Ni wangapi wanaopata huduma hafifu kwa sababu ya matatizo waliyo nayo?

Ni wangapi wanaoelewa lugha ya alama?

Ni wangapi waliofundishwa kuhusu lugha ya alama?

Je, ni nani anayetakiwa kufundishwa lugha ya alama? Viziwi peke yao, bubu pekee au na watu wote pia?

Wazazi wengi wenye watoto wenye changamoto za kusikia na kuongea bila shaka hushindwa kwa kiasi kikubwa kuwasilisha ujumbe kwa watoto wao na pia watoto wanaweza kushindwa kutoa maoni yao juu ya mambo mbalimbali ya kifamilia, kitaaluma, na mengine mengi.

Ni hakika kwamba hatupaswi kuridhika na kuendelea kuvumilia kuishi na kundi hili angali tumetengwa na pazia zito la lugha ya wasiliano na kundi hili. Nimekuja na mawazo ya namna ya kukabiliana na tatizo hili.

Ni lazima iwepo kwenye mitaala ya shule za msingi na sekondari kama ambavyo wanafunzi wanajifunza lugha nyingine mashuleni.

Huko vyuoni, ni lazima walimu waandaliwe kujua lugha hii ili waweze kuwafundisha wanafunzi wao. Lengo ni ili kila mtu awe na uwelewa wa lugha ya alama.

Kwenye taasisi nyeti za kutolea huduma kwa wananchi, ni vyema kama wangekuwepo wataalam wa lugha ya alama, au kwa kila wilaya, awepo mmoja atakayehudumia wilaya nzima kulingana na uhitaji wa huduma hii.

Akiwepo Mtlmu mmoja angekuwa msaada mkubwa kwa wengine kuelimisha na kufundisha watu wengine wengi Zaidi.

Serikali, mashirika binafsi na watu wenye nia njema dhidi ya kundi hili tuchukue nafasi zetu kujali, kuonyesha upendo, na pia kuwajibika katika kutatua changamoto kwa ndugu zetu.

SULUHISHO LA KITEKNOLOJIA

Tupo kwenye ulimwngu wenye maendeleo makubwa sana ya sayansi na teknolojia. Teknolojia imekuwa msaada mkubwa katika kutatua matatizo.

Kulingana na takwimu za Shirika la Umoja wa Mataifa, Zaidi ya watu milioni 72 wanahitaji lugha ya alama ili kufanikisha shughuli zao za kila siku na bila shka kwa hapa Tanzania, Zaidi ya watu laki 7 wanauhitaji mkubwa wa lugha hii

PROGRAM YA ViSIBLE

Ni program ya kufikirika inayoweza kuwaunganisha watu wanaozungumza lugha mbili tofauti. Mfano, anayezungumza lugha ya alama na anayezungumza lugha nyingine hususan Kiswahili au Kiswahili kutafsiriwa kuwa lugha ya alama kwa kutumia kamera ya simu au kamera iliyofungwa kwenye mfumo wa tarakilishi.

Program hii itakapokamilika itaweza kutumika mahospitalini, mahakamani, mashuleni, au kwingineko itakapohitajika. Itasaidia sana kuongeza uelewa kwa watu wengi kuhusu lugha ya alama.

Itarahisisha sana mawasiliano kwa pande zote mbili na pia itapunguza gharama za kuwalipa wakalimani katika kutasiri lugha. Kwa bahati nzuri, progmam hii itakuwa na uwezo wa kufundishwa lugha mbalimbali na hivyo kusaidia hata mawasiliano baina ya watu wanaozungumza lugha mbili tofauti.

Kitakachofanyika ni kwamba, mzungumzaji wa kwanza hufikisha ujumbe kwenye ubongo wa program hii, na kwa kutumia kamisi iliyotengenezwa ndani ya mfumo huu, itarudisha taarifa hiyo hiyo kwa lugha itakayochaguliwa, eidha kwa njia ya sauti, au ishara.

Hakutakuwa na udanganyifu wala upotoshaji kwa namna yoyote ile isipokuwa kama mfumo wake utakuwa umepewa taarifa zenye dosari.

Pia itakuwa na uhitaji wa nyenzo za kawaida sana ambazo zinapatikana katika mazingira yetu ya kila siku, kwa mfano. Simu janja.

Changamoto katika kuunda mfumo huu ni kwamba, itahitaji muda mrefu hadi kukamilika kwake.

Pia wajuzi wa wa kusuka mifumo ya komputa watahitajika kukamilisha mpango huu wa kiteknolojia.

Ninaamini hakuna kinachoshindikana katika ulimwengu huu bali palipo na nia hakika pana njia ya kufikia malengo. Mwisho wa mambo yote ni mwanzo wa mambo mapya.

Wote wenye nia ya kuziba pengo hili la kimawasiliano katika lugha wanakaribishwa katika kukamilisha projekti hii itakayokuwa yenye msaada kwa watu wengi hapa Tanzania na ulimwenguni kote.

Turejeshe furaha kwa wote, tuzibe mapengo kwa umoja wetu.

Chanzo Lugha ya alama Tanzania, Toleo la kwanza.jpg
 
Upvote 2
Back
Top Bottom