X_INTELLIGENCE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2014
- 10,400
- 14,339
"Siku ya tukio la kifo cha Sokoine mvua ilikuwa inanyesha wakati msafara wake ulipoondoka mjini Dodoma. Gari la polisi lilikuwa linaongoza msafara wake hivyo hapakuwa na wasiwasi wa usalama kwani gari zote tulizokuwa tunazipita zilikuwa zimeegeshwa pembeni mwa barabara.
Baada ya kuvuka mto Wami, kilomita kama 40 mashariki ya Morogoro, zilipita kama dakika 5, ghafla kilisikika kishindo kikubwa cha mgongano wa vyuma. Gari la Waziri Mkuu Sokoine lilikuwa limegongana na gari aina ya Landcruiser lililokuwa likiendeshwa na mpigania Uhuru wa Afrika Kusini kupitia Chama cha African National Congress (ANC), Dumisani Dube (23).
Baada ya ajali, Waziri Mkuu Sokoine maisha yake yakawa yameishia hapo. Kama kuna binadamu wenye uwezo wa kuota siku yao ya kufa, basi Sokoine ni mmoja wao kwani Jumatatu April 9 alikwenda kusali katika kanisa la Mtakatifu Paul mjini Dodoma. Usiku wa Jumanne, siku mbili kabla ya kufa kwake aliandaa karamu ya chakula kwa wakuu wa Mikoa na Mawaziri waliokuwa wamehudhuria kikao cha Bunge huko Dodoma.
Usiku wa Jumatano, April 11 aliandaa chakula cha usiku na Wabunge kutoka Mkoa wa nyumbani kwake Arusha. Chakula hiko ndo kilikuwa cha usiku wake wa mwisho duniani".
MWALIMU NYERERE ATANGAZA KIFO CHA SOKOINE HUKU AKIBUBUJIKWA NA MACHOZI.
"Ndugu wananchi, leo mnamo saa 7 mchana, Ndugu yetu, kijana wetu, Edward Moringe Sokoine, Waziri Mkuu wa Tanzania alipokuwa akirudi Dar es Salaam toka Dodoma, gari yake ilipata ajali, AMEFARIKI DUNIA".
Nukuu za Rais wa kwanza wa Tanzania, Mwalimu J,K Nyerere na mwandishi wa habari ofisi ya Waziri Mkuu, Accadoga Chiledi wakielezea kifo cha Waziri Mkuu, Edward Moringe Sokoine. Sokoine alizaliwa Agosti 1, 1938 katika kijiji cha Kisongo wilayani Monduli mkoani Arusha.
Alifariki dunia Alhamisi ya April 12,1984 kwa ajali ya gari mkoani Morogoro.