Zifahamu aina za injini za ndege na zinavyofanya kazi

Zifahamu aina za injini za ndege na zinavyofanya kazi

BoManganese

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2017
Posts
980
Reaction score
2,679
Injini moja ya Boeing787 Dreamliner inasukuma tani moja na robo ya hewa kwa sekunde ikiwa katika full power.

(Hesabu inasema, inachukua takribani miezi isiyopungua mitatu kwa binadamu wa kawaida kutumia kiwango hiki cha hewa)

Leo si vibaya kama tukifahamu juu juu kuhusu aina ya injini za ndege ili kila mmoja wetu asibaki nyuma sana.

Zipo ndege zenye injini 1,2,3,4,6 hadi 8 katika ndege moja.
Ndege nyingi zinaendeshwa na injini za aina 2 kwa muonekano tuliozoea.

(1)-Injini za Jeti (Zenye mfano wa pipa lililolazwa)

(2)-Injini za Propeller (Maarufu Mapangaboi)

1> MFUMO WA INJINI ZA JETI
Huu umegawanyika kutokana na 'modification' ya ufanisi na matumizi yake ambazo pia zipo katika makundi mbalimbali mfano,

*Turbojet 'PureJet' (Mfumo wa ndege nyingi za awali)

*Turbofan (Mfumo wa ndege nyingi za sasa)

*Turboshaft (Mfumo wa baadhi ya ndege za sasa mfano Helicopter n.k

*Scramjet (Mfumo ulio katika ndege za majaribio za mwendokasi mara nyingi ufanisi wake uanzia mara tano ya kasi ya sauti 'Hypersonic')

Injini za jeti zinafanya kazi kwa:

1-Kunyonya hewa mbele (suck)
2-Kukandamiza (compression)
3-Kulipua hewa iliyokandamizwa kwa kuchanganya na mafuta (Ignition)
4-Kisha inatoka/kupulizwa nyuma kwa kasi kubwa na kuisukuma ndege mbele (Thrust)
Mfano mzuri kazi ya injini hizi ni kama Puto lililopulizwa na kuachiwa hewani pasipo kuzibwa mdomo wake (Action and reaction)

Ndege nyingi za kisasa zinatumia injini aina ya 'Turbofan' (Gas driven) katika kundi la jeti ambazo zinasemakana kuwa na nguvu kubwa na ulaji mdogo wa mafuta.

(Unaweza kutambua injini hizi kwa haraka kwa kuona feni kubwa lililo mbele ya injini kwa ndani kidogo, usifananishe na mapangaboi)

Injini za 'Turbojet/Purejet' ambazo moja kwa moja zinanyonya hewa mbele zinakandamiza, kulipua na kuitoa hewa moja ya moto kwa kasi nyuma ambayo ndiyo nguvu pekee inayosukuma ndege kwenda mbele, hutumia mafuta mengi kuliko
Injini ya 'Turbofan' ambayo ni tofauti kidogo kwani feni lake linavuta na kusukuma hewa mbili nyuma huku hewa ya kwanza ikiwa ile inayoingia kwenye mfumo wa ndani ya injini ambayo unyonywa,kukandamizwa na kulipuliwa na hewa ya pili ni pale hewa ya kwanza iliyolipuliwa kabla ya kufika nje inazungusha visahani maalum 'turbine' zilizoungwa na 'shaft' kwenda kwenye feni lake mbele ambapo huzunguka pamoja na feni na kufanya livute na kusukuma nyuma hewa ya pili yenye nguvu zaidi inayopita nje ya mfumo wa injini (Bypass air) hivyo kuleta nguvu zaidi kwa kutumia mafuta kidogo.

2-MFUMO WA INJINI ZA MAPANGABOI

Mapangaboi au 'propeller' nazo zinafanya kazi kwa kutumia mapanga yake kuchota hewa mbele na kuisukuma nyuma kwa kasi na kuifanya ndege kwenda mbele.

*Pangaboi linaweza kuwa linazungushwa na 'propeller' iliyoungwa na piston za injini,

*Au kwa mapangaboi yenye injini ya 'turbo' (turbopropeller)yanazungushwa na hewa iliyolipuliwa (hii aina ya jeti engine yenye mapangaboi) kupitia visahani 'turbine' vilivyo ungwa na propela ya mapangaboi kupitia mfumo wa gear (geared turboprop)au yanayozunguka kupitia mkandamizo 'pressure' ya hewa iliyolipuliwa pasipo kuungana na chochote (free turbine).

*Pia 'turboshaft' mapangaboi yanayozungushwa na hewa iliyolipuliwa kupitia visahani 'turbine' vilivyoungana na propela ya mapangaboi moja kwa moja,pia yaweza kuwa 'Geared' au ila si 'free turbine'

Mifumo ya injini za kisasa ya mapangaboi inafanya kazi sawa na jeti (ukiacha za piston) katika mfumo wa ufuaji wa nishati na kuzitofautisha tu katika muonekano wa nje wa injini.

Injini zenye mfumo ya jeti ni fanisi zaidi kwa ndege zinazopaa anga za juu ambapo hewa ni hafifu, masafa marefu na mwendokasi hasa unaozidi spidi ya sauti 'supersonic'
Wakati,
Injini za mfumo wa Mapangaboi ni fanisi zaidi katika mwendo ulio chini ya spidi ya sauti 'subsonic', anga za chini na kati na masafa mafupi kwenda ya kati.

Tukumbuke pia injini za ndege hazina mahusiano wala kiunganishi chochote na tairi za ndege.

Tairi za ndege ni 'freewheel' na zimeunganishwa na mfumo wa 'brake' na kona tu.
Hakuna kinachozungusha tairi kutoka kwenye injini bali zinafuata uelekeo wa kule ndege inaposukumwa.

Crdts: Online, Aero book.
FB_IMG_15713981697436998.jpg
FB_IMG_15713981752041533.jpg
FB_IMG_15713981821563045.jpg
FB_IMG_15713981880099659.jpg
 
INJINI MOJA YA BOEING787 DREAMLINER INASUKUMA TANI MOJA NA ROBO YA HEWA KWA SEKUNDE IKIWA KATIKA 'FULL POWER'
(Hesabu inasema, inachukua takribani miezi isiyopungua mitatu kwa binaadam wa kawaida kutumia kiwango hiki cha hewa)

Leo si vibaya kama tukifahamu juu juu kuhusu aina ya injini za ndege ili kila mmoja wetu asibaki nyuma sana.

Zipo ndege zenye injini 1,2,3,4,6 hadi 8 katika ndege moja.
Ndege nyingi zinaendeshwa na injini za aina 2 kwa muonekano tuliozoea.

(1)-Injini za Jeti (Zenye mfano wa pipa lililolazwa)

(2)-Injini za Propeller (Maarufu Mapangaboi)

1> MFUMO WA INJINI ZA JETI
Huu umegawanyika kutokana na 'modification' ya ufanisi na matumizi yake ambazo pia zipo katika makundi mbalimbali mfano,

*Turbojet 'PureJet'(Mfumo wa ndege nyingi za awali)

*Turbofan(Mfumo wa ndege nyingi za sasa)

*Turboshaft(Mfumo wa baadhi ya ndege za sasa mfano Helicopter n.k

*Scramjet.(Mfumo ulio katika ndege za majaribio za mwendokasi mara nyingi ufanisi wake uanzia mara tano ya kasi ya sauti 'Hypersonic')

Injini za jeti zinafanya kazi kwa:

1-Kunyonya hewa mbele (suck)
2-Kukandamiza (compression)
3-Kulipua hewa iliyokandamizwa kwa kuchanganya na mafuta(Ignition)
4-Kisha inatoka/kupulizwa nyuma kwa kasi kubwa na kuisukuma ndege mbele.(Thrust)
Mfano mzuri kazi ya injini hizi ni kama Puto lililopulizwa na kuachiwa hewani pasipo kuzibwa mdomo wake.(Action and reaction)

Ndege nyingi za kisasa zinatumia injini aina ya 'Turbofan' (Gas driven) katika kundi la jeti ambazo zinasemakana kuwa na nguvu kubwa na ulaji mdogo wa mafuta.
(Unaweza kutambua injini hizi kwa haraka kwa kuona feni kubwa lililo mbele ya injini kwa ndani kidogo..usifananishe na mapangaboi)

Injini za 'Turbojet/Purejet' ambazo moja kwa moja zinanyonya hewa mbele zinakandamiza,kulipua na kuitoa hewa moja ya moto kwa kasi nyuma ambayo ndiyo nguvu pekee inayosukuma ndege kwenda mbele, hutumia mafuta mengi kuliko
Injini ya 'Turbofan' ambayo ni tofauti kidogo kwani feni lake linavuta na kusukuma hewa mbili nyuma huku hewa ya kwanza ikiwa ile inayoingia kwenye mfumo wa ndani ya injini ambayo unyonywa,kukandamizwa na kulipuliwa na hewa ya pili ni pale hewa ya kwanza iliyolipuliwa kabla ya kufika nje inazungusha visahani maalum 'turbine' zilizoungwa na 'shaft' kwenda kwenye feni lake mbele ambapo huzunguka pamoja na feni na kufanya livute na kusukuma nyuma hewa ya pili yenye nguvu zaidi inayopita nje ya mfumo wa injini(Bypass air) hivyo kuleta nguvu zaidi kwa kutumia mafuta kidogo.

2-MFUMO WA INJINI ZA MAPANGABOI
Mapangaboi au 'Propeller'nazo zinafanya kazi kwa kutumia mapanga yake kuchota hewa mbele na kuisukuma nyuma kwa kasi na kuifanya ndege kwenda mbele.

*Pangaboi linaweza kuwa linazungushwa na 'propeller' iliyoungwa na piston za injini,

*Au kwa mapangaboi yenye injini ya 'turbo' (turbopropeller)yanazungushwa na hewa iliyolipuliwa (hii aina ya jeti engine yenye mapangaboi)kupitia visahani 'turbine' vilivyo ungwa na propela ya mapangaboi kupitia mfumo wa gear(Geared turboprop)au yanayozunguka kupitia mkandamizo 'pressure' ya hewa iliyolipuliwa pasipo kuungana na chochote (free turbine).

*Pia 'turboshaft' Mapangaboi yanayozungushwa na hewa iliyolipuliwa kupitia visahani 'turbine' vilivyoungana na propela ya mapangaboi moja kwa moja,pia yaweza kuwa 'Geared' au ila si 'free turbine'

Mifumo ya injini za kisasa ya mapangaboi inafanya kazi sawa na jeti (Ukiacha za piston)katika mfumo wa ufuaji wa nishati na kuzitofautisha tu katika muonekano wa nje wa injini.

Injini zenye mfumo ya jeti ni fanisi zaidi kwa ndege zinazopaa anga za juu ambapo hewa ni hafifu,masafa marefu na mwendokasi hasa unaozidi spidi ya sauti 'supersonic'
Wakati,
Injini za mfumo wa Mapangaboi ni fanisi zaidi katika mwendo ulio chini ya spidi ya sauti 'subsonic',anga za chini na kati na masafa mafupi kwenda ya kati.

Tukumbuke pia injini za ndege hazina mahusiano wala kiunganishi chochote na tairi za ndege.
Tairi za ndege ni 'freewheel' na zimeunganishwa na mfumo wa 'brake' na kona tu.
Hakuna kinachozungusha tairi kutoka kwenye injini bali zinafuata uelekeo wa kule ndege inaposukumwa.

Crdts: Online,Aero book,
View attachment 1237133View attachment 1237134View attachment 1237135View attachment 1237136
Hongera sana kwa elimu nzuri
 
Swadactaaa maarifa Ni chakula Cha ubongo, Asante kwa elimu nzuri. Kutoka kwenye hiyo picha uliyoweka, injinu namba tatu nafikiri ndio inaendesha baadhi ya helkopta. Hapo hewa kutoka kwenye panga boy hiyo ya mbele ndio inakandamizwa ili kuinyanyua helkopa juu. Tujuze zile zenye pangaboy kubwa moja juu hewa ya kugandamizwa ili ndege ipae inatoka wapi?
tapatalk_1571412383812.jpeg
 
Mkuu
Shukrani Sana
Vp Kuhusu Helicopter
 
Mtoa mada ungekuja kutufafanulia kuhusu mfumo/design ya engine za Subaru kutumika pia Kwenye aircraft..
Ingawa wengi humu ndani watashangaa lakini hata Mimi mwenyewe nilisoma sehemu Fulani kuhusu hizi engine kuwa na uwezo wa kuchoma mafuta Kwa haraka zaidi (turbine) na kuipa engine nguvu na Kasi zaidi.

Je upekee huu WA hizi boxer engine za Subaru walikopi kutoka Kwenye aircraft engine?
Screenshot_2019-10-18-21-17-15.png
 
SAWA MKUU, HEBU NAMBIE NATAKA KUNUNA HELIKOPTA YANGU MAMBO YAKIWA MAZURI, NARUHUSIWA KUENDESHA MWENYEWE? NA KUPACK NYUMBANI KWANGU? AU LAZIMA NI PACH JNIA?
 
Ndege ndogo je yenye injini mbili. naweza jitengenezea uwanja wangu nyumbani kwangu, na kucharge watumiaji wengine wanaotaka kupata huduma hii? au mpaka uwe wa sirikali? ili kupunguza gharama za packing?
 
Shukran sana sas vp kuhusu uwezo wa izo machine unajuaje Yaan zile ndege ndogo na kubwa uwezo wake ni sawa tofaut ni idadi ya engine au ata uwezo wake pia tofaut
 
Huwa naaminia Sana hizi mambo..... Bila shaka Subaru unatumia rotary engine.... Najibu swali hapo juu
 
Gwajima ndege yake ana pack wapi?
jenaweza kutunzia helkopta yangu juu ghorofani kwangu?
 
Asante kwa elimu nzuri hii. Nami nijazie kidogo.
Wazalishaji wakubwa wa engine za ndege ulizozitaja hapo juu ni:-
  1. Rolls Royce (Uingereza)
  2. General Electric (Marekani)
  3. Pratt & Whitney (Marekani/Canada)
  4. Mitsubishi Motors (Japan)
 
Back
Top Bottom