Zifahamu Asasi za kiraia (Civil society organizations)

Zifahamu Asasi za kiraia (Civil society organizations)

Joined
Feb 5, 2022
Posts
38
Reaction score
60
1724199403535.png

Kwa muda mrefu, Asasi za Kiraia zimekuwa zikitambulika kwa majina tofauti tofauti kama vile; sekta ya kujitolea yaani “voluntary sector”, sekta isiyotengeneza faida, yaani “not-for-profit sector”, sekta ya hisani, yaani “charitable sector” au sekta ya tatu, yaani “third sector” baada ya sekta ya umma na sekta binafsi.

Wajibu wa Asasi za Kiraia
Dhana mbalimbali zinaeleza juu ya wajibu wa Asasi za Kiraia. Miongoni mwa dhana hizo ni dhana ya kwamba, nyakati za uchaguzi, vyama vya siasa hunadi sera zao (manifestos) zenye lengo la kuboresha maisha ya wananchi, lakini uboreshaji wa maisha ya wananchi lazima uende sambamba na ukusanyaji wa kodi.

Sasa inapotokea hali ya kuwa serikali inatamani kuboresha maisha ya wananchi wake kama ilivyoahidi, lakini wananchi hawana uwezo wa kulipa kodi ili kugharamia huduma kutoka kwa serikali, uhaba wa huduma hutokea, katika hali hii si serikali wala sekta binafsi inakuwa tayari kuchukua hatua, ndipo hapa Asasi za Kiraia huingia kati kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi, Muktadha huu unazifanya Asasi za Kiraia kujulikana kama sekta ya tatu yaani “Third Sector”

Asasi za Kiraia hutekeleza shughuli zake kwa kukusanya rasilimali fedha kutoka kwenye taasisi za serikali, makampuni ya kibiashara, kwa mtu mmoja mmoja n.k Mchango wa serikali kwa Asasi za Kiraia huweza kuwa ruzuku (grants), msamaha wa kodi (tax benefits) au msaada wa kiufundi. Mchango wa makampuni ya kibiashara kwa Asasi za Kiraia huweza kuwa ruzuku, bidhaa, watu wa kujitolea au huduma. Mchango wa mtu mmoja mmoja kwa Asasi za Kiraia huweza kuwa ruzuku, kujitolea muda/ujuzi, mali/wakfu n.k

Sifa za Asasi za Kiraia
Asasi za kiraia zinapaswa kuwa na sifa zifuatazo
  • Asasi za Kiraia zinapaswa kuwa na utaratibu maalum wa kujiendesha (should be structured) utaratibu huu unapaswa kuainisha malengo maalum ya kuanzishwa kwa Asasi, nafasi za uongozi wa Asasi, muda wa uongozi, majukumu ya viongozi n.k.
  • Asasi za Kiraia hazipaswi kuwa sehemu ya serikali na vyombo vyake ingawa inapokea ruzuku kutoka serikalini.
  • Fedha ipatikanayo kwenye Asasi ya Kiraia haipaswi kugawanywa kwa wanachama au waanzilishi kama faida. Isipokuwa fedha hii inapaswa kutumika kwa ajili ya kutoa huduma za kijamii.
  • Asasi za Kiraia zina mfumo wa kujiongoza zenyewe (self-governing) Asasi hizi zina uhuru wa kuchagua viongozi wao na hata kusitisha shughuli zao kwenye jamii.
  • Asasi za Kiraia ni za kujitolea. Uanachama wa Asasi za Kiarai ni hiari ya mtu. Mtu halazimishwi na sheria kuwa mwanachama wa Asasi ya Kiraia.
Mchango wa Asasi za Kiraia Kiuchumi
Kwa kipindi cha mwaka 2006 nchini Marekani, Asasi za Kiraia ziliweza kuchangia Dola bilioni 666.1 sawa na asilimia 5.0 ya GDP. Kwa upande wa Tanzania, kwa mujibu wa Foundation for Civil Society, Asasi za Kiraia kwa mwaka kipindi cha mwaka 2019 ziliweza kuchangia Shilingi za kitanzania bilioni 279 kwenye utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya jamii.

Mgawanyo wa Asasi za Kiraia
Asasi za Kiraia huweza kugawanywa katika utaratibu ufuatao;​
  • Afya (Health)
  • Utamaduni (Arts)
  • Siasa (Politics)
  • Elimu (Education)
  • Mazingira (Environment)
  • Ushawishi (Advocacy)
  • Dini (Religious)
  • Umoja wa Wataalamu (Professional Associations, Unions)
  • Sheria
  • N.k

By
OMAR MSONGA
CONSULTANT
Project Management, Strategy, Fundraising & Training
Call: +255 719 518 367
Email: omarmsonga8@gmail.com
DAR ES SALAAM
TANZANIA
 
Na vyama vya wafanyakazi navyo ni CSO japo Mara nyingi vinajinasibu na kujikomba kwa serikali
 
Back
Top Bottom