JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Browser kwa lugha ya Kiswahili huitwa Kivinjari. Hii ni programu ya Kompyuta au Simu ambayo hufanya kazi ya kupangilia, kuleta na kuonesha maudhui kutoka kwenye tovuti
Ifahamike kuwa 'Browser' ni kiungo muhimu kwa watumiaji wa Mtandao Wa Intaneti. Zifuatazo ni Browser salama zaidi;
1: Firefox: utengenezaji wa kivinjari hiki umezingatia umuhimu wa Usalama na Faragha. Aidha, toleo jipya la Firefox ambalo ni Firefox Quantum limeboreshwa kwa kuwa na kasi na rahisi kutumia
Hata hivyo, Firefox haijakamilika katika usalama ingawa inamruhusu mtumiaji kuambatanisha program za usalama
2: Iridium Browser: Hii imetengenezwa kwa kufanana na Chrome lakini usalama wake uko juu zaidi. Imetengenezwa kwa kuzingatia Usalama na Faragha kuliko Chrome
3: GNU IceCat: Hii ni program yenye urafiki na Firefox imetengenezwa na kutolewa bure na inafanya kazi ya kuulinda usalama wako. Huitaji kufanya settings za kiusalama
4: Brave: imetengenezwa kuegemea mfumo wa Chromium. Iko 'fast', imezingatia usalama, na imejengewa uwezo wa kuzuia matangazo ya mtandaoni. Aliyeitengeneza alikuwa mwajiriwa wa Mozilla ambao ni waendeshaji wa Browser ya Firefox
5: Tor browser: Hili ni toleo la Firefox lililoimarishwa zaidi. Iko taratibu kiutendaji kutokana na ukweli kwamba inamuunganisha mtumiaji na 'server' kadhaa kabla ya kufikia sehemu husika
6: Waterfox: Hiki ni kivinjari kingine ambacho watu wanaojali usalama katika mtandao wanaweza kutumia. Usalama wake umeimarishwa na imetengenezwa kufanya na Firefox
7: Pale Moon: Kivinjari hiki kwa sasa kinapatikana kwenye mifumo ya uendeshaji wa Kompyuta ambayo ni Windows na Linux. Aidha, Pale Moon inaendesha 'Search Engine' yake inayoitwa Goanna

Upvote
5