Lastbornson
Member
- Jan 21, 2018
- 87
- 49
ZIFAHAMU FAIDA 7 MUHIMU ZA KUJAMIIANA KWA KIWANGO STAHIKI.
Tendo la kujamiiana kwa walio wengi limekuwa ni tendon bora sana has a likifanywa na wenza ambao kila mmoja ana mvuto wa kimapenzi na mwenza wake. Ukiacha ile hali ya kujisikia raha isiyoelezeka ikaeleweka, lakini zipo faida nyingine nyingi muhimu katika miili ya wanaofanya tendon hilo. Zifuatazo ni faida 7 miongoni kwa sababu tele za kujamiiana ipasavyo:
1.HUKUFANYA UONEKANE MWENYE UMRI MDOGO KWA MIAKA 5 HADI 7 CHINI YA UMRI WAKO HALISI.
√ Kwa kiasi kikubwa watu ambao hujamiiana Mara nyingi (Mara 3 hadi 4 kwa wiki) huwa na mwonekano wa umri mdogo kwa miaka tajwa hapo juu kuliko umri wao halisi. Aidha kujamiiana pia husaidia ngozi kuwa laini na kuondoa mikunjo ya uso (wrinkles).Hali hii ni tofauti na wale ambao kujamiiana Mara chache.
2. HUIMARISHA AFYA YA UZAZI
√ Kwa mwanaume, kwa kadiri anavyojamiiana Mara kwa Mara ndivyo ubora wa mbegu zake huongezeka kwa kusababisha ujauzito ulio bora. Ifahamike kuwa hali hii ni kwa mwanaume ambaye huzalisha kiwango kinachotosha kusababisha ujauzito, kwani kuna wanaume wengine ambao wana tatizo la kuzalisha mbegu chache, hivyo ili waweze kusababisha ujauzito kirahisi hulazimika kukaa bila kujamiiana kwa muda mrefu ili wanakapokuja kujamiiana kiwango cha mbegu kinachotakiwa kifikie.
Kwa mwanamke, kujamiiana Mara kwa Mara kunasaidia kurekebisha homoni inayohusiana na mzunguko wa hedhi, na hivyo kurekebisha mzunguko wake na kumwezesha kushika ujauzito kiurahisi.
3. HUSAIDIA KUPUNGUZA UNENE
√ Kujamiiana kisawasawa kwa takribani dakika 30 hupunguza Karoli zisizopungua 100. Kwa nyongeza, Mitindo mbalimbali katika kujamiiana huleta matokeo mazuri zaidi kwakuwa misuli msingi zaidi ya mwili itahusika katika zoezi hilo.
4. HUONGEZA HAMU YA KUJAMIIANA ZAIDI
√ Kwa kadiri wenza wanavyojamiiana na kuridhishana katika tendo hilo, ndivyo kila mmoja wao anaongezeka kuvutiwa kufanya tena tendo hilo na mwenza wake.
5. HUONDOA/HUPUNGUZA MSONGO WA MAWAZO
√ Kujamiiana kisawasawa kunachochea mwili kuzalisha kemikali zinazofanya mtu ajisikie vizuri, miongoni kwa kemikali hizo ni pamoja na homoni iitwayo serotonin, ambayo hujulikana pia kwa jina la " the happy hormone" ; homoni hii humfanya mtu ajisikie mchangamfu na kwenye furaha; hivyo kupunguza msongo wa mawazo.
6. HUPUNGUZA UWEZEKANO WA KUPATA SARATANI YA TEZI DUME
√ Tatizo la saratani ya tezi dume kwa kawaida huwapata mwanaume waliopo katika umri wa kuanzia miaka 50. Katika umri juu mwanaume akiwa anajamiiana kwa kiwango stahiki hupunguza kwa kiasi kikubwa uwezekano wa kupata saratani ya tezi hilo.
7. HUONDOA/HUPUNGUZA TATIZO LA KUKOSA USINGIZI
√ Imeshuhudiwa Mara nyingi kuwa baada ya wenza kujamiiana na kufikia mshindo/kilele, hujihisi kuchoka na kuhitaji kupumzika/kulala. Licha ya kuwa hali hii ni kwa jinsi zote mbili, lakini hujitokeza zaidi kwa wanaume. Hivyo wenza wa kike mnashauriwa kutowalaumu wenza wenu wa kiume wanapopatwa na usingizi mzito baada ya tendo hilo, kwani wana sababu ya msingi iliyo nje na uwezo wao.
MUHIMU:
PAMOJA NA FAIDA ZOTE HIZO NILIZOELEZEA NA NYINGINE AMBAZO HAZIJAELEZWA HAPA, UNASHAURIWA KUHAKIKISHA KUWA KUJAMIIANA KWAKO KUNAKUWA SALAMA KWA KUHAKIKISHA KUWA UNAKUWA NA MWENZA UNAYEAMINIANA NAYE AU KUTUMIA KONDOMU KWA USAHII, KWANI TOFAUTI NA HIVYO, BADALA YA KUPATA FAIDA HIZI UTAJIKUTA UKIPATA HASARA NYINGI IKIWEMO MIMBA ZISIZOTARAJIWA, MAGONJWA YA NGONO IKIWEMO UKIMWI.
Asante kwa kusoma na kuelewa. Tafuta/pata Ukamilisho wa mapungufu ya maelezo/mada yangu toka katika vyanzo vinginevyo mbalimbali.
Ni Mimi Lastbornson.