Zifahamu lugha tano za mapenzi ikiwemo ya mwenza wako

Joined
Sep 30, 2024
Posts
7
Reaction score
4
Bwana Gary Chapman anatupa Code ya kumjua mwenza wako na vitu gani umfanyie ili yeye AHITIMISHE KWAMBA ANAPENDWA NA WEWE

unaweza kufanya mambo mazuri tu lakini kwake yakawa sio kitu kwa sababu tu haujajua lugha yake ya mapenzi.

Ndio utasikia "huyu mwanamke nampa kila kitu ila bado haoni kama nampenda" hapana haumpi kila kitu,unakosea Code zake.

Kitabu kinaelezea Lugha tano au MAMBO MATANO ambayo ukiyafanya yote au baadhi kwa mujibu wa lugha ya MWENZA WAKO basi ataona kweli unampenda

Fuatana na hili bandiko ili umjue mwenza wako anaangukia kwenye lugha ipi ya mapenzi..

1. WORDS OF AFFIRMATIONS
Haya ni Maneno mazuri ya kumsifia,kumpongeza ama kumshukuru kwa yale anayokufanyia.

Kama hii ni lugha ya mwenza wako basi hatoona unampenda MPAKA umsifie,umshukuru ama umpongeze kwa anayokufanyia.

2. QUALITY TIME
Huu ni muda unaompa mwenza wako yaani kwa kuwa pamoja na yeye mkiongea na ukimsikiliza kwa dhati kabisa huku ukimtazama yeye(eye contact)

Muda huu weka simu pembeni, laptop pembeni,Tv umezima yaani utayari wako wote unampa yeye (undivided attention)

Zingatia EYE CONTACT na INDIVIDED ATTENTION.

Kwa nini umtazame machoni(eye contact)?

kisaikolojia ukimtazama mtu machoni anaona unamsikiliza na anaona pia mko pamoja

Utangundua ukiongea na mtu asiyetuliza macho yake kukuangalia na akawa anatazama huku na kule basi utahisi mtu huyo hakusikilizi vyema.

Huwenda ukimpa muda mpenzi wako ukakaa nae na ukamsikikiza basi hapo ndio ataona unampenda kweli.

3. PHYSICAL TOUCH
Huu ni mgusano wa kimwili kama vile kutembea pamoja huku mumeshikana mikono, kumlaza kifuani huku mnaongea,kum'busu kumkumbatia n.k..

Ndio maana kuna mtu ukimbusu, ama kumshika mkono, ama kumkumbatia basi anatafsiri unamtaka kwa sababu hiyo ni lugha yake.

4. ACTS OF SERVICE
Lugha hii ni kumsaidia mwenza wako kufanya kazi zake kama vile unamsaidia kupika, kufua nguo, kubeba taka, kukosha vyombo n.k

Kuna watu ukiwasaidia kazi zao ndio wanahisi unawapenda, hiyo ndio lugha yao.

5. RECEIVE GIFTS
Lugha hii ni kumpa zawadi hata kama sio za gharama kama vile kumnunulia nguo, pete, kiatu, chakula maarufu, simu n.k

Kuna watu ukiwapa zawadi ndio wanahisi unawapenda,hiyo ndio lugha yao.

UTAIJUAJE LUGHA YAKE?
unaweza kujua kwa kuangalia mambo mawili ya msingi.

a) Chunguza kama anakufanyia wewe basi ujue ndio lugha yake.

-kama hukuletea zawadi basi hiyo lugha yake.
-kama anakupa muda wake basi jua hiyo lugha yake.
-kama anapenda kushikana na wewe basi hiyo ndio lugha yake.
-kama anapenda kukusaidia kazi zako basi hiyo ndio ligha yake
-kama huwa anakusifia basi hiyo ni lugha yake.

b) Lawama zake.
-kama anakulaumu haumletei zawadi basi ushaijua lugha yake.
-kama anakulaumu haumpi muda basi umeshajua lugha yake.
-kama anakulaumu humsaidii kazi umeshajua lugha yake.
-kama anakulaumu haumnunulii zawadi umeshajua lugha yake.

Kuna ambao lugha zote tano ni zao, kuna ambao lugha zao ni kadhaa,na kuna ambao lugha yao ni Moja,hivyo msome mwenza wako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…