Zifahamu sera za kudumu za CHADEMA za mambo ya nchi za nje zinazowagusa Diaspora

Zifahamu sera za kudumu za CHADEMA za mambo ya nchi za nje zinazowagusa Diaspora

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2013
Posts
11,550
Reaction score
40,697
Kwa uchache hapa nitaweka baadhi ya sera za kudumu za CHADEMA ambazo zinawagusa Diaspora moja kwa moja. Sera hizi zimekuwepo wakati wote toka CHADEMA ishike kasi hapa Tanzania na zilikuwa sehemu ya ilani ya CHADEMA kwenye uchaguzi wa 2005, 2010, 2015 na 2020.

1. URAIA PACHA
Chadema itaruhusu uraia pacha kwa misingi hii;
-haki ya kuzaliwa mtanzania haiwezi kupotea kwa namna yoyote ile.
-Mtanzania kuwa na uraia wa nchi nyingine hakupaswi kukunyima haki ya kuendelea kuwa mtanzania.
-Uraia wa Tanzania ni tunu isiyoweza kufutika kwa mzawa wa Tanzania.

2. PASI YA KUSAFIRIA (PASSPORT)
Ni haki ya kila mtanzania kupatiwa pasi ya kusafiria kadri inavyobidi au kuhitajika. Suala la urasimu, usumbufu na utozwaji wa gharama kubwa wakati wa kupatiwa passport utaondoshwa kabisa.

3. BALOZI ZA TANZANIA
Balozi za Tanzania zilizopo nchi mbalimbali zitageuzwa kuwa vituo rasmi vya kutolea huduma zote (One stop centre) za kidiplomasia sambamba na kuwaunganisha watu kijamii na kibiashara baina ya Tanzania na nchi zao. Teuzi na ajira za maafisa wa kibalozi zitafanyika kwa kuzingatia weredi, uwazi na ushindani.

4. USHIRIKI WA SIASA
Watanzania waliopo nje ya Tanzania watakuwa na nafasi sawa sawa na watanzania waliopo ndani ya Tanzania katika kushiriki katika siasa za Tanzania ikiwemo kupiga kampeni na kupiga kura kwa kadri itavyowezekana.

5. MCHANGO WA DIASPORA
Diaspora kipekee watatambulika rasmi kisheria (haki na wajibu wao) na mchango wao katika kuijenga Tanzania utalindwa na kupewa nafasi sawa sawa na watanzania wengine waliopo Tanzania.
 
Back
Top Bottom