Zifuatazo ndio sababu 5 za kutafuta ushauri wa kibiashara

Zifuatazo ndio sababu 5 za kutafuta ushauri wa kibiashara

Iziwari

Member
Joined
Jun 5, 2021
Posts
90
Reaction score
72
1. Kukosa kujiamini au kutojiamini.
Mara nyingi usipotambua mapema kuwa ndani yako ni mfanyabiashara. Huwa anakua na wasiwasi wa kuanzisha biashara yeyote. Lakini kuna njia nyingi za kupitia kabla haujaanza biashara. Na pale unapokua hauna wazo la kibiashara ni lazima upitie njia izo ili upate maamuzi yatakayo kufanya ujiamini Zaidi.

Dunia ya sasa tunayoishi. Huwa ni vizuri kutafuta elimu ya kufanya kitu kabla haujakianza. Swali ni kwamba elimu hii utaipata wapi, Na hapo utakapoipata, je itakusaidia? au itakua inakuelekeza mahali usipopajua? Kwaiyo tukiyafikiri hayo kwa makini.

Tutajikuta ni lazima tutafute ushauri kwa watu wa kuaminika na wenye mifano mingi ya mafanikio ya wale waliowashauri. Ni kimaanisha watu wenye shuhuda za walioshauriwa na kufanikiwa.

Kwaio kutojiamini ni hatua ya kwanza ya mtu yeyote kabla hajaanza biashara yake. Lakini hatua ya pili ambayo itakuongezea Imani ni kutafuta ushauri.

Na katika harakati za kutafuta ushauri lazima upate mtu thabiti na mwenye mifano ya kutosha. Ndio maana unakarishwa AA TANCH Company. Ili kupata ushauri wenye kukuwezesha kuanza biashara yako bila kuwa na wasi wasi. Kumbuka pia tunatoa ushauri kwa wale wenye mawazo ya kibiashara na wale wasio kabisa na wazo la biashara.

2. Kukosa maarifa na elimu ya kutosha.
Ukiwa kama mtu mwenye wazo la biashara. Au mtu yeyote unaetegemea kuja kuwa mfanyabiashara. Utajikuta tu, mara nyingi unahitaji mtu wa kuongea nae mara kwa mara. Kuhusu biashara yako.Ili biashara yako ianze kuonesha matunda.

Watu kama hawa ni wa muhimu sana. Na wanaweza kukushauri kitu kipya kulingana na wakati unaopitia kwenye biashara yako. Ukifikiri vizuri kuhusu ili, ni kama kusema watu wawili ni bora kuliko mmoja.

Na kuna mashirika mbalimbali yamejipanga ili kusaidia katika kukushauri. Na ukifata ushauri huo utajikuta unafanikiwa kweli kweli. Leo hii ningependa tena nikukumbushe kwamba AA tanch trading company itakupa ushauri uliokamilika na uliojaa maarifa ya kutosha yatakayo iwezesha biashara yako kusonga mbele.

Ikiwa una biashara au wazo la biashara wakati ndio huu wa kuongeza maarifa. Kwa kupata watu wa karibu wa kuongea nao.

3. Kuongeza nguvu na uwajibikaji.
Kuna usemi kwamba ‘’ukiwa na majukumu mengi ndipo unapokuwa na nguvu kubwa’’ (with great power comes great responsibility). Uwajibikaji ni tabia ambayo wengi tunapenda kuikimbia. Na matokeo ya kuacha kuwajibika ndio yanayoongeza ugumu katika kazi.

Swali ni kwamba tuwajibike katika nini?

Kujua nafasi yako katika uwajibikaji ni ngumu sana. Pale tu unapoona kama umeachwa mwenyewe. Inasemekana kitaalam ya kuwa unahitaji kupata mshauri wa karibu ili kuwa mtu mwenye kuwajibika Zaidi. Kama ilivo kwamba, wengi wetu tunapenda kujifunza kwa walio tangulia. Naam pia washauri wapo kwa kuwa walisha pitia hatua nyingi Zaidi yako.

Mara nyingi ukiona unajiuliza swali hili kwamba niwajibike katika nini. Hapa ndipo utakapo hitaji kushauriwa Zaidi kibiashara. AA tanch company inakupa ushauri wa kuhusu biashara yako ikiwa bado changa au ikiwa tayari imekomaa. Ili kukuongezea pia uwajibikaji.

4. Kugundua uwezo wako au biashara inayoendana na wewe.
Mshauri ni mtu muhimu sana kama ukiwa unawazo la biashara au hauna wazo lolote la biashara.

Swali ni kwamba utajuaje biashara inayoendana na wewe?

Mshauri anaweza kukuongezea nguvu pia ya kugundua biashara inayo kufaa. Au isiyo kufaa kulingana na jinsi wewe ulivo au mahali ulipo.

Washauri wanatumia njia thabiti za kitaalam kuangalia mahali ulipo. Au mahali unapotaka kuanzisha biashara yako. Kulinganisha na mtaji wako ili kuja na jibu sahihi kwamba ni biashara gani inayokufaa.

Mara nyingi watu hupuuzia hatua hii ya kutafuta washauri wa biashara. Lakini kwa wale ambao wamesha shauriwa wengi wao watakuambia hatua hii ni ya lazima. Hatua ya kutafuta mshauri wa biashara unayo endelea nayo au unayotaka kuianzisha. Itakufanya ugundue uwezo wako na mwishoni kujua biashara inayoendana na wewe.

5. Kuwa na umoja.
Kama inavoaminika umoja ni nguvu utengano ni udhaifu. Basi kuwa na watu wanaoweza kukushauri huwa inakuongezea nguvu Zaidi. Na kumbuka watu hawa, huwa wanaweza kujichukulia wao kama wewe ili upate mafanikio ambayo uliokuwa unayategemea.

Washauri wanapoona unataka ku kwama. Huwa wanakupa ushauri kutokana na utafiti ambao ulionesha mafanikio mapema. Na mara nyingi ushauri uliotokana na utafiti utakuongezea uwajibikaji. Pia uwajibikaji katika umoja, huwa wenye nguvu Zaidi.

Na hupelekea mfanya biashara kupata majibu na matokeo sahihi.

Mwisho.
AA tanch trading company tupo kwa ajili ya kukupa ushauri wa kibiashara. Kama una wazo la kuanzisha biashara haujui pa kuanzia. Kama una mtaji lakini haujui biashara itakayo fanya. Ili mtaji wako urudishe faida. Au kama hauna mtaji wala wazo la biashara.

Na kwa wale wenye mtaji mdogo kabisa tutembelee AA Tanch trading company tukuwezeshe kimawazo.

Pia tuna safirisha mashine na bidhaa mbali mbali kwa kiwango kizuri cha fedha.

Na ukiwa Pamoja nasi lazima utaanza kuona maendeleo mazuri katika kila unacho kifanya.
 
Back
Top Bottom