Zijue dalili saba za biashara inayoenda kufa

Zijue dalili saba za biashara inayoenda kufa

Joined
Jun 15, 2021
Posts
6
Reaction score
14
Katika ulimwengu wa biashara, ni kazi ngumu kuifanya biashara idumu na kukua kuliko kuianzisha hata kama ulianzisha kwa mabilioni ya pesa. Biashara nyingi huanzishwa kila siku na biashara nyingi zinakufa kila siku kwa sababu mbalimbali ambazo tutazijali siku nyingine. Katika makala ya leo, nitazjadili dalili saba ambazo zinaashiria hatari ya kifo kwa biashara husika. Safiri nami katika uzi huu tujali pamoja.

I: Kukimbiwa na wafanyakazi
Jambo la kuondoka wafanyakazi ni la kawaida katika biashara yoyote, lakini kama mwendendo huo umekuwa mkubwa basi jua kuna jambo linalohatarisha uhai wa biashara. Maana inawezekana kabisa wafanyakazi hawaoni future yoyote katika ofisi yako na morali wao wa kazi umekwisha kabisa. Chukua hatua haraka.

II: Kupungua kwa pesa iliyo katika mzunguko
Hii ni dalili mbaya sana, maana itakufanya ushindwe hata kilipia gharama mbalimbali za uendeshaji wa biashara. Biashara iliyochangamka maana yake ni pesa inaingia na kutoka kwa kasi. Pesa ikiingia na kuchelewa kutoka ni tatizo na pesa ikitoka na kuchelewa kuingia ni tatizo kubwa zaidi. Ikitokea pesa zinapungua katika mzunguko wa biashara yako, kaa chini jiulize tatizo ni nini? Inawezekana bei zako ni kubwa sana hivyo hupati wateja au inawezekana bei ni ndogo sana inakula mtaji. Pengine kuna shida kwenye marketing au kuna wezi ndani ya ofisi na wakati mwingine ni matumizi mabaya ya pesa ndani ya ofisi. Hakikisha unajua chanzo ni nini na tafuta suluhu ya tatizo hilo.

III: Matatizo ya dharula yasiyoisha kwenye biashara
Ni kawaida kwa biashara yoyote kuwa na matatizo ya hapa na pale, lakini hapa tunazungumzia matatizo ambayo yamefugwa au yameachwa kwa muda mrefu mpaka imefikia mwisho inabidi utatuzi wake uwe ni wa dhalula kama kuzima moto. Kukiwa na matukio hayo ya kujirudia sana, ni ishara kwamba biashara inapambana (struggling) kujiendesha, na inaweza kufa muda wowote.

IV: Kupotea kwa wateja
Huduma mbaya katika biashara hukimbiza wateja, na biashara bila wateja sio biashara tena, ni hobby. Katika biashara ogopa sana kumpoteza mteja, katika sanaa ya biashara mteja ndio boss mkuu. Biashara inayopoteza wateja ni biashara inayojihukumu hukumu ya kifo. Jenga utamaduni wa kujua mrejesho wa wateja wanasemaje kuhusu huduma na bidhaa zenu. Maana itakugharimu sana kuwarudisha wateja walioondoka.

V: Kupoteza hamu/shauku (passion) na biashara yako
Dunia ina mengi hususani katika kada ya biashara. Yawezekana likatokea jambo litakalokufanya uchukie au upoteze hamu ya kufanya biashara unayoifanya. Jambo ambalo kila ukiiona biashara yako inakukumbusha uchungu wa jambo hilo. Ikifikia hapo biashara hiyo iko mashakani sana, itahitajika cancelling kubwa kwa mtu huyo ili kuirudisha hamu yake ya kufanya biashara hiyo.

VI: Kufanya makosa ya kujirudia
Kila mtu anafanya makosa, hakuna aliye mkamilifu kwenye biashara. Kama si leo basi kesho utafanya makosa fulani. Lakini kwa biashara ambayo ina makosa yanayojirudia rudia ni dalili ya kuonyesha kwamba biashara hiyo ina matatizo ya msingi ambayo yasipotatuliwa yanahatarisha uhai wa biashara. Jambo la kwanza ni kujitahidi kuzuia makosa ya kizembe, na endapo kosa lolote likitokea kuwe na mifumo ya kutambua makosa haraka na kuyapatia ufumbuzi kabla athari zake hazijasambaa sana.

VII: Biashara inayosahaulika au isiyozungumzwa na watu
Biashara isiyozungumzwa ni biashara mfu ama biashara bubu. Ndio maana makampuni mbalimbali yako tayari kuwekeza mabilion ya pesa kwenye matangazo ili biashara zao zizungumzwe na watu. Biashara isipozungumzwa inasahaulika na matokeo yake haraka sana utayaona kwenye mauzo. Kwa hiyo matangazo hayana mwisho, yanaendelea katika kipindi chote cha uhai wa biashara.

Karibu tujadili pamoja, karibu kwa maswali, maoni na ushauri ili tuelimike kwa pamoja. mimi ni mchokoza maada, nategema kupata maoni zaidi kutoka kwenu. Katika makala ijayo tutazungumzia hatua tano za ukuaji wa biashara.

......... Karibuni sana! ............
 
Hahahhahah hapo ndio utaelewa kwanini watu wanapambania kuwa wagonga meza kwenye jengo tukufu Idodomya
Mkuu maisha ya kupokea kila mwisho wa mwezi mishahara na miposho yana raha yake mkuu.

Ila ndo hivyo tu
 
Mkuu maisha ya kupokea kila mwisho wa mwezi mishahara na miposho yana raha yake mkuu.

Ila ndo hivyo tu
Comment hii imenifikirisha sana! Kuna watu wanadai katiba mpya wakati huo huo wanafikiri vyeo kama RC, RAS, DC, DAS, DED havina umuhimu. Unafikiri hao watu ambao kwa sheria ya sasa ni miongoni mwa waamuzi wa katiba mpya watakubali wakae benchi bila kupokea mishahara kila mwezi na miposho? Naamini katika katiba mpya, idadi ya majimbo itabidi kupunguzwa ikiwa pamoja na marupurupu ya wabunge, je, wabunge watakubali wajinyonge? safuher nakubaliana nawe mia kwa mia
 
Kuna kitu huwa hatukiangalii kwa sababu ni rahisi kukisahau. Kutokuwa na visibility na biashara yako. Yaani unakuta ukimkurupua mtu usingizini ukaanza kumuuliza mtu maswali juu ya biashara yake anabaki katoa macho. Nitakuja na article soon, kwa sasa tunapika dawa ya tatizo.

Stay tuned!
 
Kuna kitu huwa hatukiangalii kwa sababu ni rahisi kukisahau. Kutokuwa na visibility na biashara yako. Yaani unakuta ukimkurupua mtu usingizini ukaanza kumuuliza mtu maswali juu ya biashara yake anabaki katoa macho. Nitakuja na article soon, kwa sasa tunapika dawa ya tatizo.

Stay tuned!
Tuned
 
Tunaendelea kupata michango mbalimbali. So far, comments zote ni nzuri. Ningependa nisisitize vitu vichache tu.

i. Ni ukweli wa wazi kwamba biashara ni ngumu sana, ina changamoto nyingi sana, na kwa bahati mbaya wengi wetu hatujalelewa kwenye mindset ya biashara tangu tukiwa wadogo. wengi tuliambiwa soma uwe daktari, soma uwe engineer, nk. Ndio maana watu wanao ongoza kufeli kwenye biashara ni wasomi.

ii. Pamoja na ukweli kwamba biashara ni ngumu na zina changamoto nyingi, lakini lazima tufanye biashara. ni sawa na mtu mwenye kiu kali na anaambiwa maji yaliyopo si salama, unaweza kupata magonjwa ya tumbo. Sasa huwezi kufa kwa kiu kwa sababu unaogopa ukinywa hayo maji utapata magonjwa ya tumbo, Utakunywa tu, Kama tumbo litafura utameza flagil.😂😂😂

Naendelea kualika wachangiaji, tuendelee kutoa maoni yetu.
 
Kuna kitu huwa hatukiangalii kwa sababu ni rahisi kukisahau. Kutokuwa na visibility na biashara yako. Yaani unakuta ukimkurupua mtu usingizini ukaanza kumuuliza mtu maswali juu ya biashara yake anabaki katoa macho. Nitakuja na article soon, kwa sasa tunapika dawa ya tatizo.

Stay tuned!
Karibu sana
 
Biashara inahitaji uangalizi wa karibu pia ujue kila shilingi inavyotumika.shida yetu ni kuwa mtaji mdogo majukumu mengi.hapo lazima biashara ife.
 
Biashara inahitaji uangalizi wa karibu pia ujue kila shilingi inavyotumika.shida yetu ni kuwa mtaji mdogo majukumu mengi.hapo lazima biashara ife.
Ni kweli. Hususani biashara mpya. Unapoanzisha biashara na unategemea kula na matumizi yako yote hapo hapo ni shida. Lazima ipate muda wa kutosha kustabilize.
 
Back
Top Bottom