Zijue faida muhimu za mmea wa Bamia (Okra)

Zijue faida muhimu za mmea wa Bamia (Okra)

chama mpangala

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2015
Posts
549
Reaction score
841
Screenshot_20221022-092017.png
Screenshot_20221022-092055.png

🥕1. Awali ya yote, ukichukua majani ya bamia ukayachoma kwenye moto na ukachukua yale majivu ukayapaka kwenye ngozi au kidonda ni tiba ya vipele na allergy kwenye ngozi.

🥕2. Halikadhalika ukichukua bamia mbichi ukawa unatafuna pamoja na mdimu kila siku asubuhi kama ulikuwa na kinyama kwenye mlango wa choo(Anus/Puru) kalichotokana na ugonjwa wa Bawasiri kanaweza kukauka chenyewe.

🥕3. Kama una ujauzito na unapanga siku ya kujifungua usipate shida ya mtoto kupita, kula sana mlenda wa bamia kila siku. Itakusaidia kujifungua salama na kwa urahisi.

🥕4. Ikiwa wewe ni mwanaume na mbegu zako ni nyepesi mfano wa maji maji hazina uwezo, basi jitahidi kula bamia pamoja na karanga (au korosho) wiki tatu zaweza kuwa nyingi sana utaona matokeo chanya ambapo zikiingia popote zinatungisha mimba.

🥕5. Kama wewe ni mtu mwenye vidonda au hauna vidonda vya tumbo na unataka usije kuvipata, kula kwa wingi bamia, ule mlenda wake unazuia pia Saratani ya tumbo.

🥕6. Kama wewe ni mwanamke na uke wako ni mkavu sana, hivyo kwenye tendo la ndoa unachubuka na kuumia kula bamia.

🥕7. Kama ulikuwa hujui bamia pia inasaidia kuongeza Cd4 na zingine Cd8, kama alikuwa hujui Cd8 ni kinga za Saratani ndiyo maana ukila kwa wingi bamia hasa wanawake huwezi kuugua saratani (cancer) ya titi au uzazi (Breast Cancer and Cervical Cancer).

🥕8. Kwa wagonjwa wa Kisukari ambao wao wakila bamia kwa kufululiza huwapa ahueni kubwa kwani hutuliza sukari vyema kwenye mwili kwa ufanisi mkubwa.

🥕9. Bamia huongeza uwezo wa nguvu za tendo la ndoa, kwa wasiyoelewa, bamia ni jamii ya tunda la kola ambalo jamii hizi zina wingi wa zinki na kumbuka kazi ya zinki ni kuongeza nguvu za stamina kwa tendo la ndoa, huboresha afya za mbegu za uzazi, maziwa kwa wakina mama wanaonyonyesha na pia kusafisha njia ya mishipa iliyopooza au kulegea n.k.

🥕10. Bamia husaidia kusawazisha kiwango cha tindikali mwilini (neutralize acids). Kama inavyoweza kueleweka miili yetu ilivyoumbwa imewekewa kiwango kwenye kila kitu, kwahiyo ikitokea tindikali ikazidi hupelekea maradhi mbalimbali ikiwemo vidonda vya tumbo n.k.

🥕11. Bamia husaidia kukuepusha na ugonjwa wa Anaemia (upungufu wa damu/kupungukiwa damu).

🥕12. Bamia huongeza uteute kwenye maeneo ya maungio ya mifupa yaani joints, hasa kama utakuwa unakula mara kwa mara kama sharubati, supu, mboga au mlenda.

🥕13. Kama ulikuwa hujui bamia pia husaidia kukuepusha na kupatwa na vichunusi (pimples) na husaidia kuboresha na kuinawirisha ngozi ya mwili.

🥕14. Vilevile bamia huboresha na kuimarisha afya ya mapafu na kutibia maradhi nyemelezi ya mapafu na kusaidia mfumo bora wa upumuaji.

🎯La kuzingatia zaidi upishi wa bamia utafaa zaidi ukiupika zikiwa zina ukijani wake kwa maana vile viini lishe muhimu vinavyohitajika mwilini viweze kufyonzwa hupatikana ilihali zikiwa na ukijani wake sio zikiwa zimebadili rangi kwahiyo ukipika au kuchemsha jitahidi zisibadili rangi ili kukupa mwili wako faida lukuki na kufanikiwa kwa hilo inashauriwa usizifunikie wakati zinaiva na zisichukue muda wa zaidi ya dakika saba kuiva kuepuka kuungua na kusinyaa wala kujaa maji. Halikadhalika, ikiwa zitakatwa katwa vipande vidogo itarahisisha sana kwenye zoezi la kuiva haraka na kubaki na ukijani wake wenye umuhimu kwa kuwa na viini lishe
 
Asante kwa somo zuri.

Vipi kuhusu mwenzie, Nyanya chungu(Okwa)?
 
Back
Top Bottom