John Magongwe
Member
- Jan 4, 2024
- 71
- 119
Zijue Furushi za Baraka Zinazotokana na Kutoa Sadaka
Sadaka ni nini
Sadaka ni kitu au fedha ambazo hutolewa na mtu kwa kuwapa wale aliowakusudia kama ishara ya kuwathamini na kuwapenda. Ni shukrani na maombi yetu kwa Mungu wetu. Sadaka inatolewa kwa ajili ya kushukru jambo fulani au inatolewa kuomba kutendewa jambo fulani. Inatolewa kama shukrani kwa ajili ya kujiunganisha na Mungu katika yale uliyotendewa au katika yale unayotamani kutendewa.
Ni muhimu kusema kitu cha thamani kitolewacho kwa Mungu. Yaani kwa thamani ya ulinzi, nguvu, rehema, upendo wa Mungu kwetu. Bila shaka hatuwezi kutaja vitu vyote ambavyo Mungu anatutendea, lakini, sadaka haitakiwi kuwa kitu dhaifu, masalia au kitu cha ziada tu, bali lazima liwe fungu jema kwa sababu sadaka yenyewe hueleza mbele za Mungu jinsi tunavyompenda kupitia utoaji wetu.
Kwa nini tunapaswa kutoa sadaka
Sadaka ni mali ya Mungu: Walawi 27:30 ‘Zaka ya kila kitu kutoka shambani, ikiwa ni nafaka kutoka kwenye ardhi, au tunda kwenye miti, ni mali ya Bwana, ni takatifu kwa Bwana. Hapa Biblia inasema wazi kuwa zaka ya kila kitu kutoka shambani au sehemu yoyote, iwe kwenye ardhi au kwenye miti ni mali ya Mungu. Hivyo vyote tulivyo navyo ni mali ya Mungu. Kwa hiyo wewe mtoto wa Mungu unapaswa kutoa sadaka kwa moyo ili ujiunganishe na madhabahu ya kimungu kwa ajili ya kuchota baraka zako.
Sadaka ni ukombozi na upatanisho: Walawi 16:20 “Aroni atakapokuwa amemaliza kufanya upatanisho kwa ajili ya Patakatifu pa Patakatifu, Hema la Kukutania na madhabahu, atamleta mbele yule mbuzi aliye hai. 21 Ataweka mikono yake miwili juu ya kichwa cha mbuzi aliye hai na kuungama juu yake uovu wote na uasi wa Waisraeli pamoja na dhambi zao zote, kisha kuziweke juu ya kichwa cha huyo mbuzi. Atamwachia huyo mbuzi akimbilie jangwani kwa uangalizi wa mtu aliyepewa wajibu huo. 22 Yule mbuzi atachukua juu yake dhambi zao zote mpaka mahali pasipo na watu na yule mtu atamwachia akimbilie jangwani.
Sadaka huondoa magonjwa: Sadaka unayotoa inapaswa ifanye kazi kubwa sana katika maisha yako, ikiwemo kukuondolea magonjwa yote na kukufanya kuwa huru. Wengi wameteseka sana, lakini wanapotoa sadaka na kuisemea maneno, kuwa iondoke na haya magonjwa niliyonayo, inafanya kama ulivyosema, maana sadaka inaongea kuliko kitu chochote.
Kuna nguvu za kipekee iliyo ndani ya sadaka, ambayo watu wengi hawaifahamu
Mungu anaweza kweli akawa ni Rafiki yako mkubwa sana. Anaweza kweli akawa anazungumza na wewe, na ukaisikia sauti yake, ikikwambia, nimekusikia mwanangu na nitakupa kitu fulani. Lakini ukashangaa kitu hicho hujakipata, japokuwa alikuahidi kabisa atakuwa na wewe. Hiyo ni kutokana na kuwa ulichomwomba Mungu, hukukiambatanisha na sadaka.
Kuna watu ambao walimwomba Mungu sana, na Mungu akawasikia na kuwaahidi kuwa anatakuwa nao, lakini majibu yalikuja tofauti na walivyotarajia, hadi pale walipogundua kuwa tatizo ni sadaka.
Tuangalie mifano michache kuhusu kutoa sadaka na kutotoa sadaka.
Mfano wa maombi kutojibiwa kwa kutotoa sadaka
Vita kati ya wana wa Israeli na ndugu zao wa Benyamini (Waamuzi 20:22-29)
Hii ni kuhusu wana wa Israeli siku ile walipotaka kwenda kupigana na ndugu zao Benyamini kutokana na wao kuwa na tabia ya uovu wa wazinifu, bila kuwaadhibu. Hivyo vita vikapangwa dhiki yao na Waisraeli wengine wote waliosalia, Israeli wote walimwomba Mungu aende nao ili wakawapige Benyamini. Mara ya kwanza, Mungu akawajibu akawaambia nitakuwa pamoja nanyi, nanyi mtashinda, Lakini walipokwenda walipigwa mapigo makubwa sana.
Wakamrudia Mungu wakamuuliza tena, je, utakwenda pamoja nasi mara hii nyingine? Mungu akawaambia, ndiyo nitakuwa pamoja nanyi, lakini walipoenda wakapigwa tena, wakafa watu wengi kweli.
Wakamrudia tena Mungu kwa mara ya tatu. Lakini safari hii hawakumrudia mikono mitupu, walimrudia kwa kufunga, na kwa sadaka nyingi sana, jambo ambalo hapo Mwanzo hawakulifanya. Kisha, wakamuuliza Mungu tena, je, utakwenda pamoja na sisi. Ndipo Mungu akawaambia, hakika nitakwenda pamoja na nyie. Na kweli. Walipokwenda, waliwapiga Wabenyamini wengi sana, wakatoka na ushindi mnono. Hapo ndipo walipojua nguvu ya sadaka.
Mifano ya baraka zinazotokana na kutoa sadaka
Katika kitabu cha Matendo ya Mitume 10:30-31: tunsoma habari za Kornelio ambaye kupitia sadaka alizokuwa anatoa, Mungu alimtuma malaika kuja kwake kwanza kumthibitishia kuwa utoaji wake unakumbukwa mbele za Mungu, lakini pia kupitia kumbukumbu hiyo, Mungu akamwelekeza njia sahihi ya kuurithi ufalme wa mbinguni. Tunajifunza kuwa sadaka tunazotoa kwa uaminifu zina nguvu ya kutuombea rehema kwa Bwana. Kornelio alipata rehema hii kupitia utoaji wake wa sadaka.
Katika kitabu cha Mwanzo 8:20-21: tunaona nguvu ya sadaka aliyotoa Nuhu baada ya gharika. Kutokana na uzuri wa sadaka ile, Mungu aliahidi kutoipiga tena dunia kwa gharika.
Katika kitabu cha Mwanzo 22:16-18: hapa tusoma jinsi ambavyo Mungu anamwapia Ibrahimu juu ya baraka zisizo na kipimo, ambazo Ibrahimu anaapiwa na Mungu kupitia utoaji ambao haukuwa wa kawaida, pale Ibrahimu alipokubali kumtoa mwanae wa pekee awe sadaka ya kuteketezwa sawa sawa na maagizo ya Mungu.
Katika kitabu cha 2Wafalme 4:8-17: tunasoma habari ya mwanamke wa Shunemu ambaye alikaa muda mrefu bila kupata mtoto, lakini alipata mtoto baada ya kutoa sadaka iliyompendeza Mungu. Tunaona jinsi ambavyo huyu mama alivyojitolea kumtambulisha Elisha mbele ya mume wake. Siyo jambo rahisi mtu mke kumpeleka mtu wa jinsi tofauti kwa mume wake, lakini huyu mama aliweza. Kujitoa kwake hakukupita bure; alipata mtoto. Tunajifunza kuwa yapo majibu ya maombi yetu yanayosubiri tujitoe kwa Bwana kikamilifu kisha tutapokea mahitaji yetu.
Katika kitabu cha Marko 14:9: tunasoma utoaji wa sadaka yenye thamani ya dinari 300 (sawa na mshahara wa mwaka mzima, wakati ule) ambayo Mariamu alitoa kwa Yesu. Sadaka hii ilionekana kumpendeza Yesu na akatamka neno juu ya Mariamu. Tunajinza kuwa kumbe sadaka inaweza kusababisha Mungu kusema jambo juu ya maisha yako.
Katika kitabu cha Marko 12:42-44: tunaona Yesu anavyoifurahia sadaka ya mama mjane ambaye alitoa sadaka ndogo sana machoni pa wanadamu, lakini ilikuwa kamilifu machoni pa Bwana. Hapa tunajifunza kuwa, kumbe wakati wa utoaji wa sadaka Yesu huwa yupo na huwa anachunguza sadaka zetu. Kila mmoja wetu naamini angetamani Yesu aifurahie sadaka yake na ni hakika kwamba, kama sadaka ikitolewa kwa ukamilifu, Mungu huwa anaifurahia na kutamka neno juu ya hiyo sadaka.
Katika kitabu cha 2Mambo ya Nyakati 31:10: tunaona habari za Azaria kuhani, akieleza jinsi ambavyo watu wa Mungu walivyobarikiwa pale walipoanza kutoa sadaka nyumbani mwa Bwana. Hapo awali watu hao hawakutoa sadaka kikamilifu, lakini walipoanza kutoa kikamilifu waliziona baraka za Bwana.
MAMBO YA KUZINGATIA
Umekuwa ukimwomba Mungu akupe kitu fulani, na muda mrefu umepita bila kupata majibu. Bila shaka sasa umefahamu kanuni za kupokea au kutopokea kutoka kwa Mungu. Kumbuka kuwa Mungu hana shida na fedha zako, kwa sababu vyote ni mali yake. Alikwishasema hivyo, lakini anataka kuona mtu anayemwomba anao moyo wa kujali. Hicho tu (Hagai 2:8).
Unapomuomba Mungu akupe, au akutendee jambo lo lote, hakikisha kwa uwezo ulio nao, ambatanisha sadaka yako, tena iliyo NONO ya hicho unachomwombea. Usiombe tu Mungu nipe, gari, nipe nyumba, nipe mtoto, nipe hiki, nipe kile, lakini wewe huna mpango wa kumtolea Mungu sadaka. Ukiwa na tabia hiyo majibu yako yatakuwa ni ya kuchelewa sana.
Wapo watu wanajisikia wivu kutoa sadaka nzuri eti kwamba zitaliwa na mtumishi wa Mungu. Utambue kuwa kama mtumishi wa Mungu wako anaishi kwa taabu, kwa sababu unaona vibaya kufanyika baraka kwake, uwe na uhakika kuwa baraka zako zitachelewa sana, hadi pale utakapofunguka. Utakuwa kama wale wana wa Israel walivyofunguka wakatoa sadaka kwa Mungu, ndipo waliposhinda vita dhidi ya ndugu zao wa Benyamini.
Tumeona Mungu asivyojibu maombi yetu kulingana na jinsi tusivyotoa sadaka. Pia, tumeona namna Mungu anavyomwaga baraka zake mbalimbali kufuatana na jinsi tunavyotoa sadaka.
Hivyo, ni muhimu kutoa sadaka ikiambatana na maombi yako, ili ufanikishe mambo yako, kupitia furushi za baraka mbalimbali zinazotokana na kutoa sadaka.