Zijue haki za Mpangaji

Zijue haki za Mpangaji

Joined
Aug 18, 2019
Posts
80
Reaction score
177
Katika jamii yetu ya Tanzania mpaka Sasa inakadiriwa watu wengine waishio mijini wanaishi katika nyumba za kupanga ,Hilo moja lkn kumewa na migogoro mingi Kati ya wamiliki (wapangishaji) na wapangaji lkn imeonekana wapangaji wengi wakidhurumiwa na kunyanyasika na kutokana na dhuruma za wenye nyumba basi huku wao wakiwa awazijuhi haki zao.

Basi Leo ntakuletea baadhi ya haki za mpangaji Kama zilivyo orodheshwa kwenye sheria ya ardhi ya mwaka 1999 iliyofanyiwa maboresho 2001 pia ikienda sambamba na sheria ya usajiri wa ardhi sura 334 na kesi mbalimbali.

1. Haki ya kutumia nyumba,. Ikiwa mpangaji amelipa Kodi Kama inavyotakiwa pamoja na kufwata masharti yaliyo wekwa kwenye kwenye. Mpangaji huyo apaswi kubughuziwa kwa namba yeyote ile hii imetajwa chini ya kifungu Cha 88(1) (a) Cha Sheria ya ardhi sura 133.

2. Haki ya kupata nyumba yenye hali nzuri ya kuishi binadamu. Kipindi chote cha mkataba mwenye nyumba anapaswa anaifanyia nyumba yake maboresho pale ipatapo itirafu na kuhakikisha nyumba hiyo inafaa kwa matumizi ya kuishi binadamu.. mfano Kama nyumba imebomoka ,maji yamekatwa kwa uzembe wa mmiliki Basi ni jukumu lake kuhakikisha nyumba inarudi kwenye hali yake ya kawaida kuhakikisha anaweza binadamu akaishi. Hii imetamkwa bayana chini ya kifungu Cha 88(1)(d) Sheria ya ardhi sura 113.

Ikiwa hakuna maboresho yeyote ndani ya miezi sita Basi mpangaji anaweza kudai fidia kwa mujibu wa madhira yaliyomfikia.

3. Haki ya KUPEWA notes kabla ya kusitishiwa mkataba au kufukuzwa. Hapa ngoja nikazie kumekuwa na unyanyasaji mkubwa unaotekelezwa na wenye nyumba dhidi ya wapangaji ..lkn sheria inasema mmiliki anapaswa kutoa notes (reasonable) sheria ijasema ni mda gani mtu anatakiwa KUPEWA notes Ila mda inatolewa lazima unaweza kufikirika na kukubalika kwenye akili za kawaida.

Mfano umempangisha mtu nyumba miaka kumi(10) uwezi kumpaka notes ya weak moja au mwezi mmoja ili atafute sehemu nyingine labda reasonable anatakiwa apewa maybe mwaka mmoja ,,pia umempangisha mtu mwaka mzm unataka kusitisha mkataba mda reasonable ni miezi isiyopungua mitatu (03).
 
Vipi wale tunaochelewa kulipa kodi kwa wakati?

Mimi kinachoniboa ni kulipa kodi kwa miez 6 au 3 in advance hapa nadhani sheria iweke utaratibu.
 
Hawa madalali wachawi sijui nani kawapa mamlaka ya kuchukua kodi ya mwezi mmoja hata kama wewe umelipia kodi ya miezi 3.
 
Back
Top Bottom