Zijue mashine na mitambo mbalimbali inayotumika bandarini kupakia na kupakua mizigo na shehena mbalimbali

kuna SSG, hii inataka kufanana na RTG. tofauti yao ni kwamba RTG inapatikana Yard huku SSG inakua baharini kupakua mizigo ya kwenye meli especially kontena.
Sahihi, Ship to Shore Gantry Crane (SSG) hii hutumika kushusha na kupakia Container kutoka nchi kavu/melini na ina speed kubwa kuliko Harbour Mobile Crane
 
1. Mafi Trailer hii inatumika kubeba mizigo mizito kama magari,mitambo, abnormal cargo na huvutwa na Terminal Trucks (TT) iliyoungwanishwa na Goose neck.

2.Spreader
Hizi hutumika kushusha na kupakia mizigo mipana,Container, mabomba,magari na mifuko mikubwa ya Jumbo Bags.Hii huunganishwa na Mobile Crane

i).Car Discharging Spreader
Hii hutumika kushusha magari na huunganishwa na Mobile Crane wakati wa kushusha gari melini kwenye General Cargo na Meli za Container

ii).Container Discharging Spreader
Hii inatumika kushusha na kupakia Container

iii). Pipe Discharging Spreader
Hii hutumika kushusha na kupakia mabomba kwa wakati mmoja kuanzia bomba 4

iv). Jumbo Bags Discharging Spreader
Hii hutumika kupakia na kushusha mifuko mikubwa ya mizigo(Jumbo bags) kwa wakati mmoja.

3.Forklifts
Forklift hutumika kupakia na kushusha mizigo ya aina mbalimbali. Fork lift huwekewa kifaa cha kushusha au kupakia kulingana na aina ya mizigo.

Kuna forklift za kubeba Container tupu, kubeba mizigo ya kawaida,forklift za kubeba mizigo iliyokatika hali ya kuwa rolled kama coils, Forklift za kubeba bales, Forklift za kubeba magogo ya mbao(timber logs)
 
Angalia mikono yao yani milaaiiniiii softiiii lakini inajenga na kutengeneza vitu vizito balaa mitambo ya ajabu machuma mazito. Inashangaza.


Sasa cheki hapo chini iyo mikono. Kazi kudokoa dokoa tu, kuomba misaada na kuroga. Hata toothpicks iyo mikono anashindwa.
 
Terminal Truck (TT) ni horse iliyotengenezwa kwa ajili ya kuvuta mizigo na kazi nzito ndani ya Terminal kwenye bandari.

Terminal Truck ikiwa imevaa Goose neck inakuwa limited kubeba Mafi Trailer tu haiwezi kuunganishwa na low bed au flat bed trailer.

Gooseneck ikitolewa kwenye Terminal Truck hapo inaweza kuvuta trailer kama Lowbed, Flatbed, tanker trailer yeyote yenye wheel coupling(maungio ya tela)
 
Gottward ni jina Mtengenezaji wa hizo Crane kutoka Ujerumani, jina la mtengenezaji limetumika na kuzoeleka sana kwa watu. Kuna mtengenezaji mwingine anaitwa Italgru
Noma sana huo mtambo, ulitumika kuvuta gari iliyozama kwenye maji berth No.1 pale hadi nikabaki najiuliza hizo kamba zake zina urefu kiasi gani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…